Lugha Nyingine
Kuadhimisha miaka 70 ya uhusiano wa kidiplomasia, China na Afrika zaimarisha ushirikiano katika kusukuma mbele mambo ya kisasa

Hafla ya uzinduzi wa Mwaka wa 2026 wa Mawasiliano kati ya Watu wa China na Afrika ikifanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Januari 8, 2026. (Xinhua/Han Xu)
JOHANNESBURG - Mwaka huu unatimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Afrika. Katika hatua hii muhimu, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi anafanya ziara yake ya kwanza ya mwaka nje ya nchi barani Afrika, akiendeleza desturi ya kidiplomasia ambayo imedumishwa kwa miaka 36 mfululizo.
Katika ziara hiyo, Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), alihudhuria hafla ya uzinduzi wa Mwaka wa Mawasiliano kati ya Watu wa China na Afrika kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) siku ya Alhamisi.
Maendeleo ya pamoja
Kwa miongo kadhaa iliyopita, ushirikiano kati ya China na Afrika umejikita kithabiti katika maendeleo ya pamoja. Ukiongozwa na kanuni za udhati, matokeo halisi, urafiki na nia njema, pamoja na kutafuta mema na maslahi ya pamoja, ushirikiano wa pande mbili umeendelea kusonga mbele kuelekea ubora wa hali ya juu na uendelevu zaidi.
Kwenye Mkutano wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mwaka 2024, China ilianzisha au kupandisha hadhi ya ushirikiano wa kimkakati na nchi 30 za Afrika. Kutokana na hilo, China sasa ina ushirikiano wa kimkakati na nchi zote 53 za Afrika ambazo ina uhusiano wa kidiplomasia nazo.
Pande zote mbili zilikubaliana kusukuma mbele kwa pamoja ujenzi wa mambo ya kisasa katika maeneo sita na kutekeleza hatua 10 za ushirikiano, jambo ambalo lilifungua ukurasa mpya wa kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja ya hali zote katika zama mpya.
Kupitia ushirikiano wa kivitendo, pande hizo mbili zimeoanisha uzoefu wa maendeleo wa China na mahitaji ya maendeleo ya Afrika, kuhimiza ukuaji wa pamoja kupitia kunufaishana.
Kwa mfano, China imeanzisha sera ya kutotoza ushuru kwa bidhaa kutoka nchi zote za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia nayo, na kuunga mkono ujenzi au uboreshaji wa takriban kilomita 100,000 za barabara, zaidi ya kilomita 10,000 za reli, karibu madaraja 1,000 na karibu bandari 100 barani Afrika, hatua ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa mambo ya kisasa wa Afrika na maendeleo ya kiuchumi yaliyoratibiwa.

Damaris Mutinda na Feng Xudong, Mkuu wa Idara ya Uendeshaji na Usafirishaji katika Kampuni ya Uendeshaji wa Reli ya Afrika Star, mwendeshaji wa Reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi iliyojengwa na China, wakitazama kumbukumbu ya kazi kwenye Kituo cha Kutuma Treni cha Shirika la Reli la Kenya cha Reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi jijini Nairobi, Kenya, Septemba 30, 2025. (Xinhua/Yang Guang)
Peter Kagwanja, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sera ya Afrika, jopo la washauri bingwa la Afrika lenye makao yake makuu Nairobi, amesema msukumo wa China wa ujenzi wa mambo ya kisasa umekuwa hamasa kwa nchi za Kusini mwa Dunia.
Urafiki kati ya Watu na Watu
Katika miaka mingi iliyopita, mawasiliano kati ya watu yametoa uungaji mkono wa kudumu kwa uhusiano kati ya China na Afrika. Pande hizo mbili zimekubaliana kuuteua mwaka 2026 kuwa Mwaka wa Mawasiliano kati ya Watu wa China na Afrika.
Akihutubia hafla ya uzinduzi wa mwaka huo wa mabadilishano katika mji mkuu wa Ethiopia wa Addis Ababa Alhamisi wiki iliyopita, Wang alizungumzia matokeo yenye matunda na nguvu hai kubwa ya mabadilishano ya kiutamaduni na ya kati ya watu na watu wa China na Afrika.
Akitolea mfano maendeleo katika ushirikiano wa elimu ya ufundi kati ya China na Afrika, Wang ameeleza kuwa China imeshaanzisha Karakana 17 za Luban katika nchi 15 za Afrika na kutoa mafunzo kwa makumi ya maelfu ya wataalamu, ikitoa uungaji mkono mkubwa wa kiweledi kwa maendeleo ya Afrika.

Li Wenbiao (wa kwanza, kulia), mwalimu kutoka Taasisi ya Confucius nchini Djibouti, akifundisha wanafunzi lugha ya Kichina kwenye Karakana ya Luban, eneo la kufundishia la Taasisi ya Confucius, katika Mji wa Djibouti, Djibouti, Novemba 6, 2024. (Xinhua/Wang Guansen)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar Rafaravavitafika Rasata amesema kuwa taasisi za China kama vile Karakana ya Luban na Taasisi ya Confucius zimewezesha vijana wa Madagascar kuboresha ujuzi wao wa kiufundi na ustadi wa lugha ya Kichina.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



