China na Tanzania zakubaliana kutekeleza kwa pamoja mikakati ya maendeleo

(CRI Online) Januari 12, 2026

(Picha inatoka tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China.)

(Picha inatoka tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China.)

Tanzania na China zimetoa taarifa ya pamoja zikiahidi kutekeleza kwa pamoja mikakati ya maendeleo ili kuboresha maendeleo ya pamoja.

Taarifa hiyo imetolewa Jumamosi iliyopita jijini Dar es Salaam baada ya mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mahmoud Thabit Kombo na mwenzake wa China Wang Yi, aliyekuwa ziarani nchini Tanzania.

Mawaziri hao wamesifu urafiki wa jadi kati ya Tanzania na China, ambao umejengwa kwenye msingi wa kuaminiana na kuheshimiana.

Pia mawaziri hao wamepongeza utekelezaji tulivu wa mradi wa kufufua reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na kueleza utayari wao wa kuunga mkono utekelezaji wa mradi huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha