Lugha Nyingine
Kampuni kubwa ya betri ya China yafungua kituo cha nishati cha kutoa huduma baada ya bidhaa kuuzwa sokoni mjini Riyadh

Wageni wa China na Saudi Arabia wakishiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa Kituo cha kwanza cha Mashariki ya Kati cha Kutoa Huduma cha NING SERVICE mjini Riyadh, Saudi Arabia, Januari 10, 2026. (CATL/kupitia Xinhua)
RIYADH - Kampuni kubwa ya betri ya China ya Contemporary Amperex Technology (CATL) siku ya Jumamosi ilifungua Kituo cha kwanza cha Kutoa Huduma cha NING SERVICE cha Mashariki ya Kati huko Riyadh Saudi Arabia, ikiwa ni kituo chake kikubwa zaidi cha nishati nje ya China cha kutoa huduma baada ya bidhaa kuuzwa sokoni.
Kampuni hiyo imesema kituo hicho kitaongeza uwezo wake wa uungaji mkono kwa utoaji huduma baada ya mauzo ya bidhaa sokoni katika Mashariki ya Kati na kusaidia muundo wa nishati ya eneo hilo kubadilisha kuwa wa nishati safi. Habari zimesema kuwa, Kituo hicho cha Riyadh kinatoa huduma za mzunguko kamili wa wakati wote wa matumizi baada ya mauzo, ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa betri, uhifadhi, utoaji mafunzo na kuzirudisha betri zilizotumiwa.
Anbasa Kandiel, mshauri mkuu wa Wizara ya Viwanda na Maliasili za Madini ya Saudi Arabia, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba wizara hiyo inaikaribisha kampuni ya CATL na viwanda vingine vya nishati mpya vinavyoongoza kuingia, kuendesha, na kuwekeza katika nchi hiyo ya kifalme.
"Wizara inatarajia na kuzitia moyo kampuni zaidi za nishati mpya za China kuja Saudi Arabia kufanya juhudi za pamoja na nchi ya ufalme katika kusukuma mbele malengo ya Matarajio ya 2030, hasa kwa kuzidisha ushirikiano katika mabadiliko muhimu kama vile ya kaboni chache," amesema.
Amesema, nishati mbadala ni sehemu muhimu ya Matarajio ya 2030 ya Saudi Arabia, ambayo inalenga kuufanya uchumi wa nchi hiyo kuwa wa aina mbalimbali na kuhimiza maendeleo endelevu.
Bruce Li, mkuu wa usimamizi wa bidhaa baada ya kuuzwa na betri katika CATL, amesema kampuni hiyo itapanua zaidi mtandao wake wa huduma katika Mashariki ya Kati ili kuunga mkono mpito wa nishati katika eneo hilo.
"Uamuzi wetu wa kuanzisha kituo hiki mjini Riyadh si tu ni chaguo la kibiashara, bali ni dhamira ya muda mrefu," Li amesema.

Bruce Li (kulia, mbele), meneja mkuu wa bidhaa baada ya kuuzwa na usimamizi wa betri katika Kampuni ya Contemporary Amperex Technology, akielezea hali ya bidhaa za betri kwa Anbasa Kandiel (kushoto, mbele), mshauri mkuu wa Wizara ya Viwanda na Maliasili za Madini ya Saudi Arabia, kwenye Kituo cha kwanza cha Huduma cha NING SERVICE cha Mashariki ya Kati mjini Riyadh, Saudi Arabia, Januari 10, 2026. (CATL/kupitia Xinhua)

Wageni wa China na Saudi Arabia wakipiga picha kwenye Kituo cha kwanza cha Kutoa Huduma cha NING SERVICE cha Mashariki ya Kati mjini Riyadh, Saudi Arabia, Januari 10, 2026. (CATL/kupitia Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



