Lugha Nyingine
Xi Jinping ahimiza kusukuma mbele Chama kujiendesha kwa nidhamu kali na hatua halisi zaidi

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Xi Jinping, ambaye pia ni Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia mkutano wa tano wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC (CCDI), Januari 12, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)
BEIJING - Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ambaye pia ni Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CPC), jana Jumatatu wakati akihutubia mkutano wa tano wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC (CCDI) mjini Beijing ametoa wito wa kusukuma mbele Chama kujiendesha kwa nidhamu kali kwa pande zote na kufuata matakwa ya juu na hatua halisi zaidi.
Rais Xi amesisitiza kuwa ni lazima kudhibiti madaraka kwenye mfumo wa taratibu kwa njia ya kisayansi na yenye ufanisi zaidi, na kusukuma mbele mapambano dhidi ya ufisadi kwa kupata uelewa zaidi na nia thabiti zaidi, ili kutoa hakikisho lenye nguvu kwa ajili ya kutimiza malengo na majukumu ya Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030).
Rais Xi amesema kwamba mwaka 2025, Kamati Kuu ya CPC iliongeza juhudi za kuboresha mienendo ya kazi ya Chama, kushikilia nguvu ya kupambana na ufisadi, na kufikia matokeo halisi. Amesema ni lazima kudumisha msimamo imara dhidi ya ufisadi na kutokomeza vyanzo na mazingira ya ufisadi.
Rais Xi amesisitiza kwamba kutekeleza kwa vitendo maamuzi na mipango mikuu ya Kamati Kuu ya CPC ni matakwa ya kimsingi kwa ajili ya kulinda maamuzi na heshima na uongozi wa pamoja wa Kamati Kuu ya Chama. "Oganaizesheni ya chama katika ngazi zote na wanachama na maofisa wa Chama wanapaswa kutekeleza kwa vitendo halisi maamuzi na mipango ya Mkutano wa Nne wa Wajumbe Wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC," amesema, na kusisitiza kuwa kudhibiti madaraka kwenye mfumo wa taratibu ni jukumu kuu la Chama kujiendesha kwa nidhamu kali kwa pande zote.
Amesisitiza kwamba kila mtu ni sawa mbele ya sheria na kanuni, hakuna madaraka maalumu katika kufuata sheria na kanuni, na mtu yeyote haruhusiwi kwenda kinyume cha utekelezaji wa sheria na kanuni. Rais Xi amesisitiza kwamba mapambano dhidi ya ufisadi ni mapambano makubwa ambayo Chama hakiwezi kushindwa, na kabisa hakitashindwa. Amesema hali ya hivi sasa ya mapambano dhidi ya ufisadi bado ni magumu na yenye utatanishi, na kutokomeza vyanzo na mazingira ya ufisadi bado ni jukumu gumu.

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Xi Jinping, ambaye pia ni Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia mkutano wa tano wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC (CCDI), Januari 12, 2026. (Xinhua/Yue Yuewei)

Li Xi, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni katibu wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC (CCDI), akitoa ripoti ya kazi kwa niaba ya Kamati ya Kudumu ya CCDI kwenye mkutano wa tano wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC (CCDI) Januari 6, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



