Lugha Nyingine
Midoli ya farasi iliyoshonwa kwa makosa yawa maarufu kwenye Mtandao wa Intaneti wa China

Midoli laini ya farasi iliyoshonwa na mfanyakazi kwa makosa ya "Cry-Cry Horse" ikionyeshwa kwenye duka katika Mji wa Biashara ya Kimataifa wa Yiwu katika Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, Januari 12, 2026. (Picha/VCG)
YIWU - Mdoli laini wa farasi ulioshonwa kwa makosa wa Farasi wa Kulia-Lia (Cry-Cry Horse) wenye uso wa huzuni umekuwa maarufu sana hivi karibuni kwenye Mtandao wa Intaneti wa China. Katika mji wa Yiwu, kituo cha bidhaa kilichoko mashariki mwa China, oda zimeongezeka kwa kiasi kikubwa huku viwanda vikiongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya soko.
Mdoli huo uliopewa jina la “Farasi wa Kulia-Lia” (Cry-Cry Horse), awali ulikuwa ni matokeo ya kushonwa kwa makosa, lakini bila kutarajiwa uligusa mioyo ya watumiaji wa mtandao wa intaneti kwa sura yake ya huzuni ambayo ina ushawishi wa kutuliza. Hivi sasa, midoli ya farasi ya aina hiyo karibu 20,000 huagizwa kila siku.

Mfanyakazi akionesha midoli laini ya farasi iliyoshonwa kwa makosa ya "Cry-Cry Horse" kwenye duka katika Mji wa Biashara ya Kimataifa wa Yiwu mjini Yiwu, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, Januari 12, 2026. (Picha/VCG)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



