Lugha Nyingine
Somalia yafuta mikataba yote na UAE huku kukiwa na mizozo ya kidiplomasia
Somalia, imefikia uamuzi wa kufuta mikataba yote iliyosainiwa kati ya nchi hiyo na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ili kulinda mamlaka wake na ukamilifu wa ardhi ya taifa.
Baraza la Mawaziri la nchi hiyo, lililokutana Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, limefuta mikataba yote iliyosainiwa na mashirika, vyombo husika vya serikali, na mamlaka za serikali za mitaa ili kulinda umoja, ukamilifu wa ardhi, na utaratibu wa kikatiba wa taifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu, mikataba iliyofutwa inahusu ushirikiano katika bandari za Berbera, Bosaso, na Kismayo kaskazini na kusini mwa Somalia, ikirejelea ushahidi kwamba UAE imechukua hatua za kudhoofisha uhuru wa kisiasa wa Somalia.
Mawaziri hao pia wamekatiza mikataba yote iliyopo sasa ya pande mbili kati ya nchi hizo mbili, ikiwemo mikataba juu ya usalama na ulinzi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



