Lugha Nyingine
China inakaribisha kampuni za kigeni na mtaji wa muda mrefu kuendelea kupanua uwekezaji nchini China: Naibu Waziri Mkuu

Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Waziri wa Fedha wa zamani wa Marekani Timothy Geithner, ambaye sasa ni mwenyekiti wa Warburg Pincus, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Januari 12, 2026. (Xinhua/Jin Liangkuai)
BEIJING - Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng amesema kwamba China inakaribisha kampuni za viwanda za kigeni ikiwa ni pamoja na Warburg Pincus na mtaji wa muda mrefu kuendelea kupanua uwekezaji wao nchini China na kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana na China.
He, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ameyasema hayo jana Jumatatu alipokutana na Waziri wa Fedha wa zamani wa Marekani Timothy Geithner, ambaye sasa ni mwenyekiti wa Warburg Pincus.
Naibu Waziri Mkuu huyo amesema kwamba China inatekeleza kikamilifu kanuni za maelekezo zilizowekwa kwenye mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC, kufuata mapendekezo na mipango ya Mpango wa 15 wa Miaka Mitano, na kusukuma mbele ujenzi wa soko kuu nchini la kuelekea dunia nzima na kufungulia mlango vya kutosha, kupanua kithabiti ufunguaji mlango wa kiwango cha juu na kuhimiza maendeleo ya uchumi yenye sifa bora.
Kwa upande wake, Geithner ameeleza matumaini yake kuhusu matarajio ya maendeleo ya uchumi wa China, na Warburg Pincus ina nia ya kuendelea kuongeza uwepo wake kwenye soko la China na kuhimiza kwa kina ushirikiano kati ya Marekani na China katika sekta za uchumi na biashara.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



