Lugha Nyingine
ChinaVumbuzi | Ndege inayojiendesha ya usafirishaji wa mizigo ya Tianma-1000" iliyoundwa na China kwa kujitegemea yamaliza usafiri wake wa kwanza

Picha hii iliyopigwa kwenye skrini ikionyesha ndege inayojiendesha ya usafirishaji wa mizigo ya "Tianma-1000" wakati wa usafiri wake wa kwanza, Januari 11, 2026. (Xinhua/Fu Ruixia)
Ndege inayojiendesha ya usafirishaji wa mizigo ya "Tianma-1000" iliyoundwa na Kampuni ya Kundi la Teknolojia la Xi'an ASN chini ya Kundi la Viwanda vya Kaskazini la China imemaliza usafiri wake wa kwanza tarehe 11 mwezi huu. Ndege hiyo inahusisha kazi zote za usafirishaji wa mizigo, uokoaji wa dharura, na uwasilishaji wa vifaa.
Ni ndege ya kwanza inayojiendesha yenyewe nchini China yenye uwezo wa kuendana na mazingira magumu ya uwanda wa juu na kupaa na kutua kwa muda mfupi sana, na pia kubadilika kwa haraka kati ya mifumo ya usafirishaji wa mizigo na kuishusha kwa kuzidondosha bidhaa kwenye ardhi kutoka angani, kampuni muundaji wa ndege hiyo imesema.

Picha hii ya kumbukumbu isiyo na tarehe ikionyesha ndege ya "Tianma-1000" inayojiendesha yenyewe bila rubani. (Xinhua)

Picha hii iliyopigwa kwenye skrini ikionyesha ndege ya usafirishaji mizigo ya "Tianma-1000" inayojiendesha yenyewe baada ya usafiri wake wa kwanza, Januari 11, 2026. (Xinhua/Fu Ruixia)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



