Lugha Nyingine
Kampuni changa ya China yaongoza katika kiwango cha dunia cha AI inayowezesha roboti kutenda katika ulimwengu halisi

Picha hii iliyopigwa Agosti 15, 2025 ikionyesha roboti za muundo wa binadamu zikishiriki pambano la kickboxing katika Michezo ya Dunia ya Roboti za Muundo wa Binadamu Mwaka 2025 mjini Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Ju Huanzong)
HANGZHOU - Kampuni changa ya AI ya China Spirit AI imesema kwamba modeli yake ya msingi ya AI inayowezesha roboti kutenda katika ulimwengu halisi, Spirit v1.5, sasa inashika nafasi ya kwanza duniani kulingana na kiwango cha mambo ya roboti ya mazingira halisi cha RoboChallenge, ikizidi modeli inaoongoza ya Marekani.
Kwa mujibu wa jedwali la ulinganishi la RoboChallenge, Spirit v1.5 imepata alama jumla ya 66.09 na kiwango cha mafanikio ya utekelezaji wa majukumu cha asilimia 50.33, ikizidi modeli ya pi0.5 iliyotengenezwa na kampuni ya Marekani ya Physical Intelligence. Spirit AI imesema imeweka modeli hiyo na rasilimali zake husika wazi kwa matumizi ya umma.
RoboChallenge, ambayo mara nyingi hufafanuliwa na wachambuzi wa sekta kama "mtihani wa kimataifa" wa roboti, ni jukwaa la kutathimini mashine halisi ambalo linapima modeli za AI katika mazingira halisi. Mchakato wake wa upimaji unajumuisha majukumu 30 yanayohusiana na shughuli za kila siku, ikiwemo uwekaji wa vitu, utambuzi wa malengo na matumizi ya zana.
Mbali na kupata alama ya juu zaidi kwa jumla kwenye jukwaa hilo, Spirit v1.5 pia ilikuwa modeli pekee iliyofikia kiwango cha mafanikio kinachozidi asilimia 50, kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa hadharani.
Kampuni hiyo ilianzishwa mjini Hangzhou, mji mkuu wa Mkoa wa Zhejiang mashariki mwa China, ambako pia kuna kampuni changa ya AI DeepSeek na kampuni ya roboti za muundo wa binadamu ya Unitree Robotics. Inajikita katika utafiti wa AI inayowezesha roboti kutenda katika ulimwengu halisi na roboti za muundo wa binadamu.
Qiu Jiefan, profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Zhejiang, amesema nafasi hiyo ya juu inadhihirisha kuwa Spirit v1.5 imeonyesha uwezo mkubwa wa jumla katika majukumu ya jumla ya roboti pamoja na utekelezaji wake katika mazingira halisi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



