Lugha Nyingine
Mwendesha Mashtaka Maalum wa Korea Kusini aomba adhabu ya kifo kwa rais wa zamani Yoon kwa shtaka la uasi

Picha hii iliyopigwa Februari 20, 2025 ikimwonyesha Yoon Suk-yeol (katikati) akihudhuria usikilizaji wa kesi yake ya kuondolewa madarakani katika mahakama ya Katiba ya Nchi mjini Seoul, Korea Kusini. (Xinhua/Yao Qilin)
SEOUL - Timu ya uendeshaji wa mashitaka wa kujiamulia inayoongozwa na Cho Eun-suk inafanya uchunguzi juu ya uasi na uhalifu mwingine wa rais wa zamani wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol, timu hiyo imeomba adhabu ya kifo kwa Yoon kwa shtaka la kupanga uasi kwa kutangaza kiharamu sheria ya kijeshi ya dharura na kwenda kinyume cha Katiba ya Nchi katika hali ambayo kutokuwepo kwa vita au kutokuwa na hali ya dharura nchini.
Vyombo vya habari nchini Korea Kusini vimeripoti jana Jumanne kwamba, Mahakama ya Eneo la Katikati la Seoul inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu kesi hiyo mwezi Februari.
Mahakama ya Eneo la Katikati la Seoul iliunganisha kesi tatu mwezi uliopita kwa washtakiwa wanane, ikiwa ni pamoja na Yoon kwa shtaka la kuongoza uasi na maofisa saba wakuu wa jeshi na polisi walioshtakiwa kwa kutekeleza majukumu muhimu katika uasi uo.
Timu hiyo ya uendeshaji wa mashtaka maalum Jumanne iliomba kifungo cha maisha kwa waziri wa ulinzi wa zamani Kim Yong-hyun, ikisema kwamba Kim alikuwa mpangaji muhimu aliyepanga na kuongoza uasi pamoja na Yoon kwa kuhamasisha jeshi, bila shaka anapaswa kubeba lawama kubwa na kukabiliwa na adhabu kali.
Sheria hiyo ya dharura ya kijeshi ilitangazwa na Yoon usiku wa Desemba 3 mwaka 2024, lakini ilifutwa saa chache baadaye na Bunge la Taifa.
Mahakama ya Katiba ya Nchi iliunga mkono hoja ya kumwondoa madarakani Yoon mwezi Aprili mwaka jana, na kumwondoa rasmi ofisini.
Kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani alishtakiwa akiwa kizuizini Januari mwaka jana kwa kuwa mtuhumiwa kiongozi wa uasi, na kumfanya kuwa rais wa kwanza aliye madarakani kukamatwa na kushtakiwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



