Lugha Nyingine
Mkoa wa Hainan wa China waripoti kuongezeka kwa biashara ya umeme wa kijani katika mwaka 2025

Picha iliyopigwa Machi 16, 2025 ikionyesha vifaa vya kuzalisha umeme kwa jua kwenye maegesho katika eneo la kielelezo la kutotoa kaboni la Boao mjini Boao, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China. (Xinhua/Pu Xiaoxu)
HAIKOU - Mkoa wa kisiwa wa Hainan, Kusini mwa China umeripoti kuvunja rekodi kwa nishati ya umeme ya kilowati-saa bilioni 14.727 katika miamala ya umeme wa kijani na cheti cha kijani mwaka 2025, kituo cha miamala a nishati ya umeme cha mkoa huo kimesema jana Jumatano.
Kituo hicho kimesema kuwa, takwimu hiyo inawakilisha ongezeko la mara 8.9 kutoka kwa kilowati-saa bilioni 1.488 zilizouzwa mwaka 2024, ikiingiza msukumo mkubwa katika maendeleo ya kijani na yenye kutoa kaboni chache ya Bandari ya Biashara Huria ya Hainan.
Kwa mujibu wa kituo hicho, kwa pamoja, miamala hiyo ilikuwa sawa na upunguzaji wa kawaida wa matumizi ya makaa ya mawe ya tani takriban milioni 5.89 na upunguzaji utoaji wa kaboni kwa tani takriban milioni 14.68.
Umeme wa kijani ni nishati inayozalishwa kwa utoaji wa kaboni karibu sifuri, na kimsingi huzalishwa kwa jua, upepo, au vyanzo vingine mbadala. Vyeti vya kijani ni uthibitisho pekee wa matumizi ya nishati mbadala, huku kila cheti kikiashiria kilowati-saa 1,000 za umeme wa kijani.
Mkoa huo wa Hainan wenye rasilimali nyingi za upepo na jua, umeharakisha mabadiliko yake ya kuwa kisiwa cha nishati safi na kuboresha utaratibu wake wa biashara ya umeme wa kijani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



