EU na nchi wanachama wa NATO Zaiunga Mkono Greenland wakati mvutano wa Arctic unapoongezeka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 15, 2026

Bonge la barafu likionekana katika Ghuba ya Disko karibu na Ilulissat, Greenland, eneo linalojitawala la Denmark, Machi 22, 2025. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

Bonge la barafu likionekana katika Ghuba ya Disko karibu na Ilulissat, Greenland, eneo linalojitawala la Denmark, Machi 22, 2025. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

OSLO - Umoja wa Ulaya (EU) na nchi wanachama wa NATO vimeongeza uungaji mkono wa kisiasa na kijeshi kwa Greenland, huku wasiwasi ukiongezeka juu ya usalama katika Arctic kufuatia taarifa ya hivi karibuni aliyotoa Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kisiwa hicho chenye umuhimu wa kimkakati.

Wizara ya Ulinzi ya Denmark imethibitisha jana Jumatano kwamba Denmark inaongeza uwepo wake wa kijeshi ndani na karibu na Greenland, ikishirikiana kwa karibu na washirika wa NATO.

Habari iliyotolewa na chombo cha habari inasema kuwa uwepo huo wa kijeshi ulioongezwa kuanzia Jumatano unahusisha uwezo wa ziada kama vile manowari, ndege na askari. Tangazo hilo lilitolewa kabla ya mkutano kati ya Denmark, Greenland na Marekani uliofanyika Washington.

Rais wa Marekani Donald Trump  akitoa hotuba kwenye Hafla ya Maandalizi (Turkey Pardoning Ceremony) ya Sikukuu ya Kitaifa ya Kutoa Shukrani kwenye Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Novemba 25, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

"Lengo ni kufanya mazoezi ya kuongeza uwezo wa kufanya operesehni chini ya hali ya kipekee ya Arctic na kuimarisha uwepo wa NATO katika Arctic, ili kusaidia usalama wa Ulaya na wa nchi za pande zote za Arctic," wizara hiyo imesema.

Vikosi vya Jeshi la Sweden vimethibitisha kwamba askari wa Sweden wapo katika kikosi cha kwanza cha kuwasili kisiwani humo.

Askari wa ulinzi akiwa zamu yake kwenye ukumbi wa mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya NATO  huko The Hague, Uholanzi, Juni 24, 2025. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

Askari wa ulinzi akiwa zamu yake kwenye ukumbi wa mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya NATO huko The Hague, Uholanzi, Juni 24, 2025. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

Norway pia imetuma askari. Kwenye mkutano na waandishi wa habari na waziri wa ulinzi wa Denmark uliofanyika jana Jumatano, Waziri wa Ulinzi wa Norway Tore Sandvik alisema kwamba Norway inatuma wanajeshi wawili kwenda Greenland kwa "kupanga mpango wa ushirikiano zaidi kati ya nchi wanachama."

Mbali na kupangilia moja kwa moja vikosi vya kijeshi, uungaji mkono wa kisiasa umeelezwa katika ngazi ya kitaifa na ya EU. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Yvette Cooper jana Jumatano alitoa wito wa kutaka NATO "kuongeza uwepo wake wa kijeshi na usalama katika Arctic," akielezea eneo hilo kuwa ni "mstari wa mbele wa ushindani wa siasa za kijiografia."

Picha hii iliyopigwa Januari 7, 2026 ikionyesha mandhari ya Aasiaat, Greenland, eneo linalojitawala la Denmark. (Picha na Zhang Quanwei/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Januari 7, 2026 ikionyesha mandhari ya Aasiaat, Greenland, eneo linalojitawala la Denmark. (Picha na Zhang Quanwei/Xinhua)

Greenland ni eneo linalojitawala ndani ya nchi ya kifalme ya Denmark, huku Copenhagen ikidumisha udhibiti wa mambo ya ulinzi na sera za diplomasia. Marekani ina kituo cha kijeshi kisiwani humo. Tangu kushika madaraka tena mwaka 2025, Trump ameelezea mara kwa mara shauku ya "kuipata" Greenland na hajaondoa uwezekano wa matumizi ya nguvu. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha