Kenya yaanza kuhifadhi mabaki ya ndovu Craig kwa njia ya ‘taxidermy’

(CRI Online) Januari 15, 2026

Tembo wakionekana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Amboseli nchini Kenya, Januari 8, 2026. (Xinhua/Xie Jianfei)

Tembo wakionekana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Amboseli nchini Kenya, Januari 8, 2026. (Xinhua/Xie Jianfei)

Shirika la Huduma za Wanyamapori la Kenya (KWS), chombo kinachomilikiwa na serikali kwa ajili ya kusimamia wanyamapori, limesema Jumanne wiki hii kwamba mchakato wa kuhifadhi kwa umbo lake halisi (taxidermy) mwili wa Craig, ndovu maarufu nchini Kenya ambaye alifariki mapema mwezi huu akiwa na umri wa miaka 54 umeanza rasmi.

Ndovu huyo aliyekuwa akitambulika sana kwa pembe zake za aina yake zenye urefu wa kugusa ardhini na, kila moja ikiwa na uzito wa kilo zaidi ya 45, alikuwa akiishi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Amboseli katika Kaunti ya Kajiado na alikuwa mmoja wa ndovu wachache wenye pembe hizo za aina yake waliosalia barani Afrika.

Shirika hilo limesema limechukua hatua ya kuuhifadhi mwili wa ndovu huyo kwa umbo lake halisi kwa madhumuni ya elimu, kisayansi, na maonyesho ya umma.

Craig, ambaye aliishi katika hifadhi hiyo ya Amboseli kwa zaidi ya miaka 50 alifariki Januari 3, 2026 akiwa na umri wa miaka 54 kutokana na kujikunja kwa utumbo mkubwa.

Craig atakuwa ndovu wa pili maarufu kutoka mbuga hiyo ya Amboseli kuhifadhiwa kwa njia hiyo ya taxidermy, baada ya tembo mwingine aliyeitwa Tim, aliyefariki mwka 2020 akiwa na umri wa miaka 50.

Tembo wakionekana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Amboseli nchini Kenya, Januari 8, 2026. (Xinhua/Xie Jianfei)

Tembo wakionekana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Amboseli nchini Kenya, Januari 8, 2026. (Xinhua/Xie Jianfei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha