Lugha Nyingine
China yachangia vifaa vya matibabu kwa Burundi
Ubalozi wa China nchini Burundi umechangia vifaa vya matibabu kwa serikali ya Burundi jana Alhamisi ili kuisaidia nchi hiyo kutimiza malengo ya maendeleo endelevu na dira yake ya maendeleo.
Hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo ilifanyika jana katika Hospitali ya Prince Regent Charles mjini Bujumbura, mji mkuu wa kibiashara wa Burundi, ambayo ni moja ya hospitali zitakazonufaika na vifaa hivyo, pamoja na Hospitali Kuu ya Gitega, katikati mwa Burundi, na Hospitali ya Mpanda iliyoko mkoa wa Bujumbura, magharibi mwa nchi hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Umma nchini Burundi, Pierre Sinarinzi amesema, vifaa hivyo vinalenga kupunguza mzigo wa raia wa Burundi ambao wanakabiliwa na changamoto zinazohusiana na vifaa duni vya afya.
Naye Kaimu Balozi wa China nchini Burundi Fang Guoqing amesema, mchango huo unahusisha vipengele 244 vya dawa na vipengele 288 vya vifaa vya matibabu, kwa lengo la kuboresha huduma ya afya kwa raia wa Burundi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



