Kenya yatarajia ukuaji wa mauzo ya nje baada ya kufikia makubaliano ya kibiashara na China

(CRI Online) Januari 16, 2026

Kenya Alhamisi ilisema inatarajia ukuaji wa mauzo ya nje baada ya China kutoa asilimia 98.2 ya soko la ushuru-sifuri kwa bidhaa kutoka nchi hiyo chini ya makubaliano ya kutotoza ushuru yaliyotangazwa hivi karibuni.

Waziri wa uwekezaji, biashara, na viwanda wa Kenya Lee Kinyanjui amesema hatua hiyo muhimu inafuatia makubaliano kati ya nchi hizo mbili baada ya China kutangaza mwezi Juni mwaka 2025 ufikiaji wa bila kutozwa ushuru kwa bidhaa zinazotoka nchi za Afrika.

“Kuanzishwa kwa ufikiaji huria kwa ushuru-sifuri kutafungua uwezo mkubwa wa kiuchumi kwa wafanyabiashara wa Kenya wanaouza bidhaa nje, ikiongeza aina za bidhaa zinazouzwa nje, hasa kwenye sekta ya kilimo.” Kinyanjui amesema kwenye taarifa iliyotolewa mjini Nairobi, akiongeza kuwa hatua hiyo pia inatarajiwa kuipatia Kenya nafasi nyingi za ajira.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha