ChinaVumbuzi | China yaonesha kwa umma roboti ya uchimbaji chini ya bahari kwa kuhimiza utafiti kwenye kina kirefu cha bahari

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 16, 2026

Wafanyakazi wakiandaa uendeshaji wa majaribio wa roboti ya kwanza ya chini ya bahari iliyoundwa na China kwa kujitegemea yenye uwezo wa kufanya uchimbaji wa 3D na ufuatiliaji wa papo hapo (in-situ monitoring) ndani ya tabaka la chini ya bahari katika Bahari ya Kusini ya China, Oktoba 14, 2025. (Idara ya Utafiti wa Jiolojia ya Baharini ya Guangzhou/kupitia Xinhua)

GUANGZHOU - Roboti ya kwanza iliyoundwa na China kwa kujitegemea yenye uwezo wa kufanya uchimbaji wa 3D na ufuatiliaji wa papo hapo ndani ya tabaka la chini ya bahari imekamilisha kwa mafanikio uendeshaji wa majaribio katika Bahari ya Kusini ya China kwenye kina cha mita 1,264 chini ya bahari.

Roboti hiyo, iliyoundwa na Idara ya Utafiti wa Jiolojia ya Baharini ya Guangzhou (GMGS) chini ya Idara kuu ya Utafiti wa Jiolojia ya China, imefikia malengo yote wakati wa majaribio yake ya hivi karibuni, ikionesha mafanikio makubwa katika uwezo wa China wa kufanya utafiti kwenye kina kirefu cha bahari na uwezo wa kufanya ufuatiliaji wa papo hapo ndani ya tabaka chini ya bahari kwenye muundo maalumu wa ardhi, GMGS imesema Jumatano wiki hii.

"Inaweza kuchimba huria na kujiweka kwa usahihi kwenye miundo ya kina kirefu ya bahari. Inaweza kujikwepa miamba na vifusi vya viumbe huku ikipanga njia nzuri zaidi inayofaa kwa kujongea," amesema Zhu Yangtao, mhandisi wa GMGS ambaye pia ni naibu kiongozi wa mradi huo wa roboti.

Ameongeza kuwa, kwa kuwa imefungwa vitambuzi vingi, roboti hiyo inaweza pia kufanya ufuatiliaji wa papo hapo wa muda mrefu, wa maeneo mapana, wa kupata data za pande nyingi ndani ya tabaka chini ya bahari.

Zhu amesema wakati wa majaribio hayo, mfumo wa roboti ulifanya ufuatiliaji wa ndani wa miundo ya bahari ya kina kirefu kwa wakati halisi, ukikamata seti za data zaidi ya 2,000 kuhusu mkusanyiko wa methane, oksijeni iliyoyeyuka, na muundo wa tabaka.

"Data zilizopatikana zitatusaidia kuelewa vizuri hali ya kijiolojia ya eneo la uchimbaji wa majaribio," amesema.

Matabaka kwenye bahari ya kina kirefu yana maliasili muhimu kama vile hidrati za gesi, elementi adimu za bahari kuu, na noduli za polymetali. Usalama na uendelezaji wake endelevu ni muhimu sana kwa usalama wa nishati na maliasili ya nchi. Hata hivyo, utafiti wake unakumbwa na changamoto za mazingira magumu sana, ikiwemo halijoto ya chini, chumvi nyingi, shinikizo kubwa, na hali isiyo tulivu ya kijiolojia.

Picha iliyopigwa Oktoba 14, 2025 ikionyesha roboti ya kwanza ya chini ya bahari iliyoundwa na China kwa kujitegemea yenye uwezo wa kufanya uchimbaji wa 3D na ufuatiliaji wa papo hapo ndani ya tabaka la chini ya bahari katika Bahari ya Kusini ya China. (Idara ya Utafiti wa Jiolojia ya Baharini ya Guangzhou/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha