China inapenda kushirikiana na Canada ili kukuza vichocheo vipya vya ukuaji: Waziri Mkuu Li

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 16, 2026

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 15, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 15, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - China inapenda kuimarisha ushirikiano na Canada katika maeneo kama vile nishati safi, teknolojia ya kidijitali, kilimo cha kisasa, mambo ya anga ya juu, viwanda vya uzalishaji wa kisasa na mambo ya fedha, ili kukuza vichocheo vipya vya ukuaji wa uchumi, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema alipofanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney mjini Beijing jana Alhamisi.

"China inakaribisha kampuni nyingi zaidi za Canada kuwekeza nchini China na inatumai kwamba Canada itatoa mazingira ya biashara yaliyo ya haki na yasiyo ya kibaguzi kwa kampuni za China zinazowekeza nchini humo," Waziri Mkuu Li amesema.

Amesema kupitia juhudi za pamoja za pande hizo mbili, uhusiano kati ya China na Canada umeonyesha mabadiliko, ambayo yamekaribishwa sana na watu kutoka sekta mbalimbali za nchi zote mbili.

Akibainisha kwamba kudumisha maendeleo mazuri na utulivu wa uhusiano kati ya China na Canada kunaendana na maslahi ya pamoja ya nchi zote mbili, Waziri Mkuu Li amesema China inapenda kushirikiana na Canada ili kudumisha ushirikiano wa kimkakati, kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, kuheshimu maslahi ya msingi ya kila mmoja, kupanua kila mara ushirikiano wa kivitendo, na kuingiza nguvu mpya katika maendeleo ya nchi zote mbili.

Ametoa wito kwa pande zote mbili kuendelea kuunga mkono mawasiliano na ushirikiano katika elimu, utamaduni, utalii, michezo, masuala ya vijana, ushirikiano wa ngazi za chini ya serikali kuu, na kuwezesha mawasiliano kati ya watu.

"China inapenda kuimarisha ushirikiano na Canada ndani ya mifumo kama vile Umoja wa Mataifa, Shirika la Biashara Duniani, Kundi la nchi 20 na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki, kwa pamoja kulinda mfumo wa pande nyingi na biashara huria," Li ameongeza.

Kwa upande wake, Carney amesema kwamba tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, serikali ya Canada imekuwa ikishikilia kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja.

"Canada inapenda kuimarisha mazungumzo na China katika nyanja mbalimbali kwa msingi wa kuheshimiana, kutumia kikamilifu faida bora zinazokamilishana, na kuhimiza ushirikiano katika maeneo kama vile uchumi, biashara, nishati, uchumi wa kijani, kilimo, na mawasiliano kati ya watu," amesema.

Waziri Mkuu huyo amesema kampuni za China zinakaribishwa kuwekeza na kufanya biashara nchini Canada, na kampuni za Canada zikiwa na imani kubwa ya kuendelea kuimarisha ushirikiano kati yao na China.

Kabla ya mazungumzo hayo, Waziri Mkuu Li alifanya hafla ya kumkaribisha mwenzake Carney kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing. 

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 15, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 15, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha