Kaimu Rais wa Venezuela atoa wito wa mageuzi ya viwanda vya mafuta ili kuvutia uwekezaji wa kigeni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 16, 2026

Kaimu Rais wa Venezuela Delcy Rodriguez (katikati) akitoa ripoti yake ya mwaka bungeni akiwa kwa niaba ya chombo cha mambo ya utawala  huko Caracas, Venezuela, Januari 15, 2026. (Picha na Marco Salgado/Xinhua)

Kaimu Rais wa Venezuela Delcy Rodriguez (katikati) akitoa ripoti yake ya mwaka bungeni akiwa kwa niaba ya chombo cha mambo ya utawala huko Caracas, Venezuela, Januari 15, 2026. (Picha/VCG)

CARACAS - Kaimu Rais wa Venezuela Delcy Rodriguez jana Alhamisi wakati akitoa ripoti yake ya mwaka bungeni akiwa kwa niaba ya chombo cha mambo ya utawala ametoa wito kwa bunge kuidhinisha mpango wa mageuzi ya viwanda vya mafuta ili kuvutia uwekezaji kutoka nje na kuhimiza ufufukaji wa uchumi wa nchi hiyo.

Katika ripoti yake hiyo ya mwaka bungeni, Rodriguez amesema kwamba mageuzi husika yatasaidia kuboresha mazingira ya uendeshaji wa sekta ya mafuta na kuongeza uwezo wake kwa ushirikiano na nje.

Kaimu Rais huyo amesema kuwa uzalishaji mafuta wa nchi hiyo ya Amerika Kusini ulifikia mapipa milioni 1.2 mwezi Desemba mwaka jana. Amesema, mapato kutoka kwenye mauzo ya mafuta nje ya nchi yatatumika zaidi kuunga mkono ujenzi wa mfumo wa afya ya umma, kuhimiza maendeleo ya uchumi na kusukuma mbele miradi ya miundombinu.

"Venezuela kwa sasa iko katika hatua muhimu ya mabadiliko, na serikali itafanya utafutaji kuhusu njia ya kujipatia fedha za kigeni iliyo ya kufuata hali halisi zaidi na ya aina mbalimbali," amesema Rodriguez.

Ameongeza kusema kuwa, nchi hiyo inapaswa kushughulikia uhusiano wake na pande zote, ikiwemo pamoja na Marekani kwenye msingi wa kuheshimiana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha