Vikosi vya Somalia na AU vyawaua wanamgambo wa al-Shabaab zaidi ya 30 katika operesheni ya pamoja

(CRI Online) Januari 16, 2026

Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) na vikosi vya Umoja wa Afrika (AU), vikiungwa mkono na washirika wa kimataifa vimeua wanamgambo wa al-Shabaab zaidi ya 30 jana Alhamisi kwenye operesheni ya pamoja kusini mwa Somalia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Mogadishu nchini Somalia na Ujumbe wa Umoja wa Afrika wa Uungaji Mkono na Kuleta Utulivu nchini Somalia (AUSSOM), operesheni hiyo, iliyofanywa kwa njia ya anga na kuhusisha mapigano mbalimbali ya ardhini dhidi ya wapiganaji wa al-Shabaab, yalifanywa karibu na kambi ya kijeshi ya Bulunagaad katika eneo la Lower Shabelle.

"Kupitia mashambulizi yaliyoratibiwa ya ardhini na angani, wanamgambo wa al-Shabaab zaidi ya 30 wameuawa, wakati huohuo wengine kadhaa wamejeruhiwa" ujumbe huo umesema.

Kwa mujibu wa ujumbe huo, awali wanamgambo hao walikuwa wameshambulia vikosi vya SNA na AUSSOM, wakati wa operesheni za kufuatilia wapiganaji wa al-Shabaab waliobaki ambao walikimbilia mji wa pwani wa Gendershe na mhimili wa Jilib-Marka chini ya operesheni zinazoongozwa na SNA zilizopewa jina la Operesheni "Hidden Sword".

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha