App ya “Uko Hai?” yagusa pengo la usalama kwa watu wanaoishi peke yao

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 16, 2026

Hivi karibuni, App moja ya China kwenye Apple App Store inayoitwa “Uko Hai?” imefuatiliwa sana na umma. Hadi kufikia tarehe 11 Januari, App hiyo ilichukua nafasi ya kwanza katika orodha ya App za kulipia kwenye Apple App Store.

App hiyo inaundwa kama chombo chepesi cha usalama kwa watu wanaoishi peke yao na ni rahisi kutumia. Watumiaji wanatakiwa kuweka mawasiliano ya dharura, na kujisajili kila siku. Endapo mtumiaji atashindwa kujisajili kwa siku kadhaa mfululizo, mfumo utatuma barua pepe kiotomatiki kwa watu wa mawasiliano ya dharura siku inayofuata.

Umaarufu wa App ya “Uko Hai?” haueneza wasiwasi na hofu, bali kwa kuonyesha wazi hatari ambayo imekuwepo lakini iliyopuuzwa kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Saba ya China, hadi kufikia mwisho wa mwaka 2020, idadi ya familia za mtu mmoja nchini China ilikuwa zaidi ya milioni 125. Kadri kuishi peke yao kunavyokuwa hali ya maisha kwa watu wengi, kwa hiari au kwa kulazimishwa, maswali ya kuhakikisha usalama, na kugunduliwa mapema wakati dharura inapotokea hayabaki tena kuwa matatizo ya mtu binafsi, bali yanakuwa changamoto ambayo jamii nzima inapaswa kukabiliana nayo.

Katika majibu yao ya hivi karibuni, timu ya App hiyo imesema kwamba katika hatua zinazofuata za kuboresha App hiyo, wataongeza kazi za kutuma ujumbe mfupi, na kufikia kuanzisha huduma za kuandika ujumbe na kadhalika.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha