Lugha Nyingine
Mjumbe Maalum wa Rais wa China ahudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais mpya wa Guinea
Mjumbe Maalum wa Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Umma la China Bw. Zheng Jianbang amehudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais mpya wa Guinea, Mamady Doumbouya iliyofanyika Conakry, mji mkuu wa nchi hiyo juzi Jumamosi na kufanya mazungumzo naye.
Katika mazungumzo yao baada ya hafla hiyo, Rais Doumbouya amesema Guinea inathamini urafiki wa jadi na China na iko tayari kuzidisha ushirikiano wa kirafiki na China katika nyanja mbalimbali ili kupandisha uhusiano wa pande mbili hadi kufikia ngazi mpya.
Kwa upande wake, Bw. Zheng amesema China inaweka umuhimu mkubwa kwenye maendeleo ya uhusiano kati yake na Guinea, na iko tayari kushirikiana na Guinea kuendeleza urafiki wa jadi, kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana, na kuhimiza upigaji hatua kubwa zaidi katika uhusiano wa washirika wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



