Lugha Nyingine
China yaendelea kuwa mchangiaji mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa dunia
Rais wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) Bw. Borg Brende amesema, uchumi wa China unakadiriwa kuzidi ukuaji wa asilimia 5 katika kipindi cha mwaka huu wa 2026, ukionyesha uhimilivu mkubwa katikati ya changamoto duniani na kuendelea kuchangia kwa sehemu kubwa zaidi katika ukuaji wa uchumi wa dunia.
Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni na Shirika la Habari la China, Xinhua mjini Geneva, Uswisi, kabla ya Mkutano wa mwaka wa WEF 2026, Bw. Brende amesema, China si tu inaendelea kuimarisha nguvu zake katika sekta za jadi lakini pia inapanuka kikamilifu katika sekta zinazoibukia, ikichochewa na kuongezeka kwa uwekezaji katika utafiti, maendeleo na uvumbuzi.
Bw. Brende pia ameelezea imani yake katika mtazamo wa uchumi wa China, akisema kuwa kama China itaendelea kusukuma mbele mageuzi ya kiuchumi na kudumisha uwekezaji katika utafiti na ujasiriamali, itashuhudia ukuaji na ustawi wa kila mara.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



