Kenya yashawishi wawekezaji wa China ili kukuza sekta ya filamu

(CRI Online) Januari 29, 2026

Kenya inaongeza juhudi ili kuendeleza sekta yake ya filamu kwa kutafuta uwekezaji na ushirikiano na wawekezaji wa China.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Filamu ya Kenya Bw. Sudi Wandabusi, amewaambia wanahabari jana Jumatano mjini Nairobi, kuwa Kenya ina nia ya kutumia uungaji mkono wa kifedha na kiteknolojia wa China ili kujijenga kuwa kitovu cha kikanda cha uzalishaji filamu.

Akiongea kwenye tamasha la 14 la soko la filamu la Kalasha, Bw. Wandabusi amesema kupitia uzalishaji filamu wa kushirikiana na wawekezaji wa China, Kenya itaweza pia kuonyesha filamu zake katika soko kubwa la China.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha