Shirika la Ndege la Tanzania lazindua safari za moja kwa moja za ndege kwenda Ghana kuunga mkono maandalizi ya AFCON 2027

(CRI Online) Januari 29, 2026

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limezindua njia ya moja kwa moja ya ndege kutoka Dar es Salaam hadi Accra, Ghana jana Jumatano, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya kandanda ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2027 (AFCON) ambayo Tanzania itakuwa mwenyeji sambamba na nchi jirani za Kenya na Uganda.

Waziri wa uchukuzi wa Tanzania Bw. Makame Mbarawa akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa njia hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, amesema safari tatu za ndege kila wiki zitarahisisha maandalizi ya AFCON 2027, kuhimiza uhusiano wa kiuchumi, na kurahisisha usafiri kati ya Afrika Mashariki na Magharibi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa ATCL Bw. Peter Ulanga, amesema hatua hiyo inaongeza idadi ya njia zake hadi 32, na kuimarisha uwezo wake wa ushindani katika soko la kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha