Lugha Nyingine
Rais Xi awajibu Maveterani wa Vita vya Ukombozi wa Taifa la Zimbabwe
Rais wa China Xi Jinping Jumatano amewajibu Maveterani wa Vita vya Ukombozi wa Taifa la Zimbabwe.
Katika barua yake hiyo, Rais Xi amebainisha kuwa wakati wa ujana wao, Maveterani hao walijitolea kwenye jukumu kubwa la ukombozi wa taifa, wakiacha maskani zao, na kujenga urafiki na undugu mkubwa na China katika mapambano hayo.
Amesema hadi leo, maveterani hao bado wanaendelea kujitolea kwa dhati kwenye urafiki kati ya China na Zimbabwe na ule wa China na Afrika, hali ambayo inagusa mioyo ya watu.
Rais Xi amesema kwamba China iko tayari kuchukua utekelezaji wa matokeo ya Mkutano wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika kama fursa ya kuendeleza urafiki wa jadi na Afrika na kwa pamoja kujenga mustakabali mzuri zaidi wa uhusiano kati ya China na Afrika.
Pia ameelezea matumaini yake kwamba maveterani hao watawatia moyo vijana wengi zaidi wa Afrika kujitolea kwa ajili ya urafiki kati ya China na Zimbabwe na China na Afrika.
Maveterani hao walimwandikia Rais Xi hivi karibuni, wakieleza shukrani zao kwa uungaji mkono muhimu wa China katika ukombozi wa taifa la Zimbabwe, kumpongeza kwa kuongoza Chama cha Kikomunisti cha China na watu wa China kufikia mafanikio makubwa katika zama mpya, na kwa kuweka njia yenye umaalumu wa China kuelekea mambo ya kisasa ambayo inatoa maarifa muhimu kwa nchi zingine zinazoendelea.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



