Rais Macron asema hali wasiwasi ya Greenland ni "onyo la kimkakati" kwa Ulaya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 29, 2026

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (katikati) akikutana na Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen (kulia) na Waziri Mkuu wa Greenland Jens-Frederik Nielsen kwenye Ikulu ya Elysee jijini Paris, Ufaransa, Januari 28, 2026. (Picha na Henri Szwarc/Xinhua)

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (katikati) akikutana na Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen (kulia) na Waziri Mkuu wa Greenland Jens-Frederik Nielsen kwenye Ikulu ya Elysee jijini Paris, Ufaransa, Januari 28, 2026. (Picha na Xinhua)

PARIS - Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema jana Jumatano kwamba kupamba moto kwa mvutano na Marekani juu ya Greenland ni onyo la kimkakati kwa Ulaya zima, wakati huohuo amesisitiza mshikamano wa Ufaransa na Denmark na Greenland.

"Matukio ya hivi karibuni yanathibitisha kwamba hali hiyo ya Greenland ni onyo la kimkakati kwa Ulaya zima: juu ya kudumisha mamlaka yetu huru ya Ulaya, juu ya mchango wetu kwa usalama wa Arctic, juu ya kupambana na uingiliaji wa nchi za nje na habari potofu au uwongo, juu ya mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, na juu ya uhusiano wa washirika wenye upendeleo kwanza kwa ajili ya maendeleo endelevu na kupunguza hali ya kutegemea kimkakati," Rais Macron amesema kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na viongozi wa Denmark na Greenland jijini Paris.

Rais Macron amesema Ufaransa inajiunga pamoja na washirika wote wa Umoja wa Ulaya kujikita kithabiti katika kanuni za mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi na ameongeza kusema kuwa Ufaransa itaendelea kulinda kanuni hizo kwa mujibu wa Katiba ya Umoja wa Mataifa.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen ametoa wito wa kuitaka Jumuiya ya NATO ifanye kazi yake muhimu zaidi katika eneo hilo na Kaskazini ya Juu, ikiwa ni pamoja na Greenland na maeneo ya pembezoni mwake.

Greenland, kisiwa kikubwa zaidi duniani, ni eneo linalojitawala ndani ya nchi ya kifalme ya Denmark, na Copenhagen bado inadumisha udhibiti wa mambo ya ulinzi na mambo ya nje. Tangu arudi madarakani mwaka 2025, Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akieleza mara kwa mara tumainio lake la "kuipata" Greenland, lakini limekuwa likikataliwa mara kwa mara na Ulaya.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto)akimkaribisha Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen kwenye Ikulu ya Elysee jijini Paris, Ufaransa, Januari 28, 2026. (Picha na Henri Szwarc/Xinhua)

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto)akimkaribisha Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen kwenye Ikulu ya Elysee jijini Paris, Ufaransa, Januari 28, 2026. (Picha na Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha