ChinaVumbuzi |  Watafiti wa China watengeneza pacemaker ndogo zaidi yenye ukubwa wa kapsuli na uwezo wa kujiendesha yenyewe

(CRI Online) Januari 29, 2026

(Picha/CRI)

(Picha/CRI)

Timu ya utafiti ya China imetengeneza kwa mafanikio kifaa kidogo zaidi cha kusaidia moyo, kijulikanacho kitaalamu kwa jina la “pacemaker,” chenye uwezo wa kujiendesha chenyewe, mafanikio ambayo yanatengeneza njia mpya kwa ajili ya kuendeleza vifaa vya kielektroniki vinavyoweza kupandikizwa mwilini.

Mafanikio hayo ambayo yamechapishwa kwenye jarida la Nature Biomedical Engineering, yametokana na utafiti wa ushirikiano wa karibu miaka saba uliohusisha taasisi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Akademia ya Sayansi ya China, Chuo Kikuu cha Tsinghua, Chuo Kikuu cha Peking na hospitali kadhaa.

Mwandishi wa kwanza wa utafiti huo, ambaye pia ni profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha Akademia ya Sayansi ya China Ouyang Han amesema kuwa mafanikio hayo ya kiteknolojia yanaweza kurefusha muda wa kifaa hicho cha pacemaker katika kusaidia uhai wa binadamu kulingana na muda wa moyo wa asili, hivyo kutatua tatizo muhimu la kurudia kila mara upasuaji wa kupandikiza moyo.

Amesema, mafaniko hayo pia yamefungua njia mpya kuelekea matumizi ya vifaa vya kielektroniki vya kupandikizwa mwilini bila kuhitaji matengenezo katika muda wote wa maisha ya binadamu na vinavyoweza kuunganishwa kwenye mfumo wa mwili wa binadamu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha