China, Uingereza zakubaliana kuendeleza ushirikiano endelevu wa kimkakati wa pande zote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 30, 2026

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 29, 2026. (Xinhua/Li Xiang)

Rais Xi Jinping wa China na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer ambaye yuko ziarani mjini Beijing, wamekubaliana kuwa nchi hizo mbili zinapaswa kuendeleza ushirikiano wa kimkakati wa pande zote ulio endelevu na wa muda mrefu.

Katika mkutano wao siku ya Alhamisi, Rais Xi amesema wakati dunia ya leo inashuhudia mabadiliko pamoja na machafuko, China na Uingereza, zikiwa ni wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi zenye nguvu kiuchumi, zinapaswa kuongeza mazungumzo na ushirikiano ili kudumisha amani na utulivu duniani, wakati huohuo zikikuza uchumi na kuboresha maisha ya watu wao.

Akisisitiza haja ya kuangalia historia kutoka kwenye mtazamo mpana zaidi, Rais Xi ametoa wito kwa nchi hizo mbili kuvuka tofauti zilizopo na kudumisha kuheshimiana, ili ziweze kubadilisha mustakabali wa nguvu bora za ushirikiano kuwa mafanikio halisi, na kufungua wigo mpya wa uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wao na dunia nzima kwa ujumla.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Starmer amesema anafurahia kuwa waziri mkuu wa kwanza wa Uingereza kuitembelea China ndani ya kipindi cha miaka minane.

“Ziara hii, na ujumbe wa wawakilishi muhimu wapatao 60 kutoka mashirika ya biashara na ya kiutamaduni ya Uingereza, inaonesha upana wa ushirikiano kati ya Uingereza na China, na dhamira ya Uingereza ya kuimarisha kwa kina na kupanua uhusiano na China” amesema.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 29, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha