China na Uingereza zinapaswa kuendeleza "moyo wa kuvunja barafu" na kuimarisha uhusiano wa ushirikiano: Waziri Mkuu Li

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 30, 2026

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akitoa hotuba kwenye hafla ya kufunga mkutano wa Baraza la Biashara la Uingereza na China wa mwaka 2026 katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 29, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akitoa hotuba kwenye hafla ya kufunga mkutano wa Baraza la Biashara la Uingereza na China wa mwaka 2026 katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 29, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - China na Uingereza zinapaswa kuendelea kuendeleza "moyo wa kuvunja barafu" na kuimarisha uhusiano wa ushirikiano, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema kwenye hafla ya kufunga mkutano wa Baraza la Biashara la Uingereza na China wa mwaka 2026 uliofanyika mjini Beijing siku ya Alhamisi.

"Hili si tu chaguo la busara kwa nchi hizo mbili kukabiliana na hatari na kuhimiza maendeleo kwa pamoja, bali pia ni jukumu lao linalopaswa kutekelezwa kama nchi kubwa zenye kuwajibika kushughulikia kwa pamoja matatizo ya dunia," Waziri Mkuu Li amesema.

Amesema kwamba China na Uingereza ni washirika muhimu wa kiuchumi na kibiashara wenye maslahi mapana ya pamoja, na kwamba mradi pande zote mbili zitazingatia kuheshimiana, kusonga mbele katika mwelekeo mmoja, kuondoa vikwazo, na kushikilia uwazi na ushirikiano, nchi hizo mbili zinaweza kufikia matokeo ya kunufaishana na kuleta ustawi kupitia mafanikio ya pamoja.

Waziri Mkuu Li amesema kwamba mwaka jana, licha ya shinikizo la kiuchumi linaloongezeka, China imesukuma mbele maendeleo yenye sifa bora yanayoongozwa na uvumbuzi, ikionyesha uimara mkubwa na uhai wa kipekee wa uchumi wake.

Huku akisisitiza kwamba China inaanza kutekeleza Mpango wa 15 wa Miaka Mitano mwaka huu, Waziri Mkuu Li amesema kuwa jumla ya uchumi wa China itafikia kiwango kipya katika kipindi cha miaka mitano ijayo, huku muundo wake wa uchumi ukiendelea kuboreshwa na vichocheo vipya vya ukuaji vikiendelea kupanuka, jambo ambalo litatoa nafasi kubwa kwa ushirikiano kati ya China na Uingereza.

Huku akisema kwamba kampuni za nchi hizo mbili zina uwezo mkubwa wa ushirikiano, Li amesema kuwa zinaweza kuelekeza juhudi zao katika maeneo manne, kupanua "nyongeza mpya" la biashara ya pande mbili na kuendeleza biashara ya huduma kuwa nguzo mpya ya ukuaji wa ushirikiano; kuunda "injini mpya" ya maendeleo ya kivumbuzi; kuchunguza "maeneo mapya" ya ushirikiano wa pande tatu, pamoja na kuimarisha "nguvu mpya" katika mawasiliano kati ya watu, sambamba na kuendelezwa kwa miradi zaidi ya chapa inayopendwa na wananchi wa nchi zote mbili.

Waziri Mkuu wa Uingereza anayezuru China, Keir Starmer, amesema katika hafla hiyo kwamba lengo la ziara yake hiyo ni kupata uelewa mpana na wa kina zaidi kuhusu China, na kubaini na kunufaika na fursa zaidi za ushirikiano, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa Uingereza na kuunga mkono ukuaji na ustawi wa nchi hiyo.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akitoa hotuba kwenye hafla ya kufunga mkutano wa Baraza la Biashara la Uingereza na China wa mwaka 2026 kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 29, 2026. (Xinhua/Ding Haitao)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akitoa hotuba kwenye hafla ya kufunga mkutano wa Baraza la Biashara la Uingereza na China wa mwaka 2026 kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 29, 2026. (Xinhua/Ding Haitao)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha