Seneti ya Marekani yashindwa kusukuma mbele mpango wa kutengwa fedha huku kufungwa kwa sehemu za ofisi za serikali kukikaribia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 30, 2026

Picha hii iliyopigwa Novemba 5, 2025 ikionyesha jengo la Bunge la Marekani, Capitol, Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Hu Yousong)

Picha hii iliyopigwa Novemba 5, 2025 ikionyesha jengo la Bunge la Marekani, Capitol, Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Hu Yousong)

WASHINGTON - Baraza la Juu la Marekani jana Alhamisi lilishindwa kusukuma mbele mpango wa kutengwa kwa fedha kutokana na migongano kuhusu sera ya uhamiaji, hali ambayo inaongeza hatari ya kufungwa kwa sehemu za ofisi za Serikali Kuu.

Baraza hilo la juu lilipiga kura 45-55 kwenye upigaji kura wa kiutaratibu, likishindwa kufikia kura 60 zinazohitajika ili kusukuma mbele mpango wa kutengwa fedha ulioidhinishwa na Baraza la Chini.

Kwa kuwa wabunge wa chama cha Democrat wakishikilia viti 47 katika Seneti, matokeo ya upigaji kura yanaonyesha kuwa Wabunge kadhaa wa chama cha Republican pia wamepiga kura kupinga mpango huo.

Matukio mawili vya hivi karibuni ya vifo vya watu kutokana na kufytuliwa risasi yaliyotokea katika Jimbo la Minneapolis yamewafanya Wabunge wa Democrat kutafuta njia ya kubadilisha uendeshaji wa mashirika ya uhamiaji. Kiongozi wa wabunge hao wa Democrat walio wachache katika Seneti Chuck Schumer alisema Jumatano wiki hii kwamba hadi Idara ya Utekelezaji wa Sheria wa Uhamiaji na Forodha (ICE) itakapodhibitiwa kwa kiasi cha kufaa na kufanyiwa mageuzi kwa pande zote kwa kupitia utungaji wa sheria , mpango wa kutengwa fedha wa Wizara ya Usalama wa Ardhi ya Nchi (DHS) hautaweza kupitishwa kwenye Seneti.

Kiongozi wa wabunge wa Republican walio wengi kwenye Seneti John Thune amesema kwamba "ataweka machaguo" kufikiria pia kupitisha miswada mingine mitano ya kutengwa fedha wakati akifikiria azimio la muda mfupi la kutengwa fedha kwa mfululizo la wizara ya DHS.

Wizara ya DHS na kitengo chake ICE vitaweza kufanya uendeshaji wa kimsingi bila kusita hata kama fedha zao zitaondolewa kutoka kwenye bajeti ya mwaka, kwa sababu Muswada Mmoja Mkubwa Mzuri (One Big Beautiful Bill) -- muswada mkubwa wa kodi na matumizi ulioidhinishwa Julai 2025 -- ulitoa dola takriban bilioni 178 kwa wizara ya DHS.

Schumer alielezea madai ya wabunge wa Democrat Jumatano wiki hii, ikiwa ni pamoja na kukomesha doria za kuzunguka mitaani, kufuata kwa makini zaidi kanuni za ukaguzi, kuweka kanuni zamienendo inayoweza kutekelezwa, kuwataka askari wa serikali kuu kufuata vigezo sawa vya matumizi ya nguvu kama ilivvyo kwa vyombo vya utekelezaji wa sheria vya maeneo husika, pamoja na kutekeleza sera ya "kutovaa vinyago vya kuficha sura, na kuvaa kamera mwilini" kwa askari wa serikali kuu.

Hata kama makubaliano yatafikiwa, muswada huo utalazimika kupitishwa na Baraza la Juu na Baraza la Chini, ambalo liko mapumzikoni wiki hii hadi Jumatatu.

Mvutano huo unatishia kuitumbukiza nchi hiyo katika kufungwa kwingine kwa serikali kuu miezi miwili tu baada ya kufungwa kwa siku 43 -- muda mrefu zaidi katika historia ya Marekani.

Wizara nyingi za Marekani, ikiwa ni pamoja na Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya na Huduma za Kibinadamu, Wizara ya Kazi, Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi na Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji, yatashuhudia fedha zao zikiishia kuanzia kesho Jumamosi.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha