Wataalamu Wachina watoa mafunzo ya magonjwa ya kitropiki visiwani Zanzibar, Tanzania ili kuadhimisha Siku ya NTD Duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 30, 2026

Mtaalamu mchina akionyesha namna ya kufanya uchunguzi wa kichocho kwa kutumia hadubini katika Kisiwa cha Pemba cha Zanzibar, Tanzania, Januari 28, 2026. (Timu ya wataalamu wa mradi wa kuzuia na kudhibiti kichocho Zanzibar unaosaidiwa na China/kupitia Xinhua)

Mtaalamu mchina akionyesha namna ya kufanya uchunguzi wa kichocho kwa kutumia hadubini katika Kisiwa cha Pemba cha Zanzibar, Tanzania, Januari 28, 2026. (Timu ya wataalamu wa mradi wa kuzuia na kudhibiti kichocho Zanzibar unaosaidiwa na China/kupitia Xinhua)

DAR ES SALAAM - Timu ya wataalamu wa mradi wa kinga na tiba ya kichocho Zanzibar unaosaidiwa na China imeandaa shughuli ya uenezi na utoaji wa mafunzo ya kupima, kuthibitisha na kutibu magonjwa katika Kisiwa cha Pemba visiwani Zanzibar, Tanzania ili kuadhimisha Siku ya Mwaka 2026 ya Magonjwa ya Kitropiki Yaliyopuuzwa Duniani.

Watu zaidi ya 200 walishiriki kwenye shughui hiyo siku ya Jumatano, wakiwemo maofisa visiwani kutoka sekta za afya, maji, kilimo na elimu, pamoja na wafanyakazi wa afya wa mitaani na wakazi wa huko.

Wang Wei, kiongozi wa timu hiyo ya wataalamu Wachina, amesema shughuli hiyo inaweka mkazo katika elimu ya afya ili kuhimiza ushiriki wa jamii na kupunguza hatari za maambukizi kutoka kwenye chanzo.

Ameongeza kuwa wataalamu hao pia walitoa mafunzo mahsusi kuhusu namna ya kupima ili kuthibitisha ugonjwa wa kichocho (schistosoma haematobium), wakiunganisha mafunzo ya kinadharia na mazoezi halisi ili kuongeza usahihi wa kugunduliwa na kuthibitishwa mapema kwa magonjwa.

Huku akifafanua kuwa kudhibiti magonjwa ya kitropiki yaliyopuuzwa duniani ni muhimu sana kwa usawa wa afya na heshima ya binadamu, Wang ametoa wito wa kuendelea kuhimiza huduma za afya kwa wote kwa kupitia juhudi za kuboresha upatikanaji wa maji salama ya kunywa na majengo ya usafi, kuboresha usafi wa mazingira, kuimarisha elimu na uenezi wa mambo ya afya, na kuhamasisha ushiriki mpana wa kijamii.

Masoud Suleiman, mratibu msaidizi katika Wizara ya Afya Kisiwani Pemba, ameipongeza China kwa msaada wake huo wa kiufundi wa muda mrefu.

Suleiman ameeleza kuwa wataalamu wa China wametoa mipango inayoweza kutekelezwa na kupata matokeo halisi katika ufuatiliaji, kujenga uwezo wa kupima na kuthibitisha magonjwa na mikakati ya kuzuia magonjwa, na kuimarisha kwa ufanisi mfumo wa huduma ya afya ya msingi ya visiwani humo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha