Lugha Nyingine
Tanzania yatoa wito wa kuandaliwa miongozo ya kisera kuharakisha matumizi ya magari yanayotumia umeme
Tanzania imetoa wito wa kuandaliwa kwa miongozo ya kisera iliyo wazi na nyumbulifu ili kuhimiza matumizi ya teknolojia ya magari yanayotumia umeme (EV) na kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi.
Katibu Mkuu katika ofisi ya makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi ametoa kauli hiyo jana Alhamisi baada ya kupokea nyaraka za mwongozo wa kiufundi wa sera kutoka kwa Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia ya Tanzania (COSTECH).
Muyungi amesema Tanzania inahitaji kuweka mazingira wezeshi ya kiusimamizi na kutoa motisha ili kuhimiza uwekezaji binafsi katika miundombinu ya magari yanayotumia umeme. Amebainisha kuwa matumizi ya magari yanayotumia umeme yatasaidia kuhimiza uhifadhi wa mazingira, yakiungwa mkono wa uwezo unaoongezeka wa uzalishaji umeme wa nchi hiyo.
Pia amezihimiza taasisi za kiufundi kuimarisha mafunzo ya kitaalamu ili kujenga uwezo wa ndani katika sekta hiyo ya magari yanayotumia umeme.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



