Waziri wa mambo ya nje wa China afanya mazungumzo ya kimkakati na Katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Russia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 02, 2026

Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Kamati kuu ya chama, akikutana na Sergei Shoigu, Katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Russia, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 1, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Kamati kuu ya chama, akikutana na Sergei Shoigu, Katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Russia, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 1, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

BEIJING - Mwanadiplomasia Mkuu wa China Wang Yi amekutana na Sergei Shoigu, Katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Russia, mjini Beijing siku ya Jumapili, ambapo alimkaribisha Shoigu kufanya ziara nchini China kwa ajili ya mazungumzo ya kimkakati kwa mujibu wa uteuzi wa Rais wa Russia Vladimir Putin.

Wang, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya chama, amesema kuwa dunia inazidi kushuhudia mabadiliko makubwa na misukosuko, huku utaratibu wa kimataifa wa baada ya Vita vya Pili vya Dunia na kanuni zinazosimamia uhusiano wa kimataifa vikiathiriwa pakubwa, na dunia ikikabiliwa na hatari halisi ya kurejea kwenye sheria ya msituni.

"Zikiwa ni nchi kubwa na wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN), China na Russia zina jukumu na wajibu wa kutekeleza mfumo wa kweli wa pande nyingi, kulinda mfumo wa kimataifa huku Umoja wa Mataifa ukiwa kiini chake, kutetea dunia yenye ncha nyingi iliyo sawa na yenye utaratibu, pamoja na utandawazi wa kiuchumi wenye manufaa ya pamoja na jumuishi, na kufanya kazi ya kujenga mfumo wa usimamizi duniani ulio wa haki na wenye mantiki zaidi," Wang amesema.

Akibainisha kuwa China na Russia ni majirani wakubwa wa kila mmoja na washirika wa kimkakati wa pande zote wa uratibu katika zama mpya, Wang amesema nchi hizo mbili zinapaswa kudumisha mawasiliano ya karibu kuhusu masuala makubwa ya uhusiano wa pande mbili, kuongeza kuungana mkono katika masuala yanayohusiana na maslahi ya msingi ya kila mmoja, na kulinda maslahi yao yenyewe na ya pamoja.

Wang amesema China inapenda kushirikiana na Russia ili kutekeleza kikamilifu maafikiano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kuzidisha uratibu wa kimkakati, na kufungua matarajio mapya ya uhusiano kati ya China na Russia katika mwaka mpya.

Kwa upande wake Shoigu amesema kwamba mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 25 tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Ujirani Mwema na Ushirikiano wa Kirafiki kati ya Russia na China, na kwamba uhusiano kati ya nchi hizo mbili unajengwa juu ya msingi wa kuheshimiana, kuaminiana, usawa na kunufaishana.

Amebainisha kuwa tangu kuanza kwa mwaka huu, dunia imeshuhudia hali tata na misukosuko, huku masuala ya usalama na maeneo tete yakizuka mara kwa mara.

"Russia imekuwa ikishikilia kwa dhati kanuni ya kuwepo kwa China moja, inafuatilia kwa karibu hatua za vikosi hasimu vinavyolenga kudhoofisha utulivu wa pande zote za Mlango-Bahari wa Taiwan, na inapinga kithabiti majaribio ya Japan ya kuharakisha kurejesha tena mwelekeo wa umilitarizm," Shoigu amesema.

Amesema, Russia inapenda kuendelea kuungana mkono kithabiti na China, kuimarisha ushirikiano wa pande mbili, na kuimarisha uratibu ndani ya mifumo ya pande nyingi kama vile Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, na BRICS.

Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya chama, akikutana na Sergei Shoigu, Katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Russia, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 1, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya chama, akikutana na Sergei Shoigu, Katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Russia, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 1, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha