Lugha Nyingine
Rwanda yaadhimisha Siku ya Mashujaa ya Kitaifa
Rwanda Jumapili iliwaenzi mashujaa wa taifa katika maadhimisho ya Siku ya 32 ya Mashujaa ya Kitaifa kote nchini.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akiambatana na Mke wake Jeannette Kagame waliweka shada la maua katika Mnara wa Mashujaa wa Kitaifa uliopo katika Remera, Wilaya ya Gasabo ya Kigali, ambapo walikaa kimya kwa muda wakiwakumbuka mashujaa hao.
Maafisa waandamizi wa serikali, wanadiplomasia, na familia za mashujaa waliopoteza maisha yao wa Rwanda pia walishiriki katika sherehe hiyo inayofanyika Februari Mosi kila mwaka, ambapo kwa mwaka huu ipo chini ya kaulimbiu "Ushujaa na Umoja kwa Maendeleo ya Rwanda".
Akizungumza katika tamasha lililofanyika Jumamosi usiku jijini Kigali kama sehemu ya sherehe hizo, Jean-Damascene Bizimana, waziri wa umoja wa kitaifa na ushiriki wa raia wa Rwanda, alitoa wito wa kuwataka Wanyarwanda kuenzi mashujaa walioanzisha taifa hilo, walioopoteza maisha yao wakitetea uhuru wa taifa, waliopigania uhuru wa taifa, na walioikomboa Rwanda kwenye ukandamizaji na dhuluma.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



