Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa Ethiopia Azindua Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Nishati ya Upepo Uliojengwa na Kampuni ya China

Picha hii ya kumbukumbu isiyo na tarehe ikionyesha mandhari ya Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Nishati ya Upepo cha Aysha II katika Jimbo la Somali, Ethiopia. (Kampuni ya Umeme ya Dongfang/kupitia Xinhua)
ADDIS ABABA - Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Jumamosi alizindua mradi wa kipindi cha kwanza wa Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Nishati ya Upepo cha Aysha II katika Jimbo la Somali, akisisitiza kwamba maendeleo ya nishati safi ni kiini cha kazi ya muda mrefu ya kubadilisha mundo wa uchumi wa nchi hiyo.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi, ambayo ilihudhuriwa na Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, Abiy amesema Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Nishati ya Upepo wa Aysha II kinaonyesha juhudi za Ethiopia za kufikia malengo ya kujitegemea kupitia utumiaji mzuri wa maliasili ya nchi hiyo.
"Ninapenda kutoa shukrani zangu kwa Kampuni ya Umeme ya Ethiopia (EEP), Kampuni ya Umeme ya Dongfang ya China inayobeba ujenzi wa mradi huu, na watu katika eneo hili kwa mchango wao katika kukamilisha kwa mafanikio ujenzi wa mradi wa kipindi cha kwanza," amesema Abiy.
Amesema kuwa maendeleo ya nishati safi nchini Ethiopia yatahimiza utandawazi wa uchumi wa kikanda na mafungamano ya kuvuka mipaka, Abiy amesema hatua za Ethiopia kuelekea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nishati haviwezi kuhakikishwa bila ushirikiano na nchi jirani.
Mradi huo wa Aysha II ambao ujenzi wake ulianza mwaka 2017, utakuwa na jumla ya uwezo uliofungwa wa kuzalisha umeme wa megawati 120 (MW), huku umeme wa megawati 80 kutoka mradi wa kipindi cha kwanza ukiwa tayari umeshaunganishwa kwenye gridi ya taifa, kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa EEP Ashebir Balcha.

Picha hii ya kumbukumbu isiyo na tarehe ikionyesha mandhari ya Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Nishati ya Upepo wa Aysha II katika Jimbo la Somali, Ethiopia. (Shirika la Umeme la Dongfang/kupitia Xinhua)

people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma