Lugha Nyingine
UN waonya dhidi ya mvutano unaoongezeka katika Tigray, Ethiopia
(CRI Online) Februari 02, 2026
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Jumamosi ameonya dhidi ya kuongezeka kwa mvutano katika Jimbo la Tigray nchini Ethiopia, na kuzitaka pande zote kujizuia na kutatua hali ya kutokubaliana kwa kupitia njia na mazungumzo ya amani yanayolenga kujenga kuaminiana.
Akizungumza katika taarifa yake, Farhan Haq, naibu msemaji wa Guterres, amesema katibu mkuu huyo anafuatilia kwa karibu hali mpya katika Tigray, ambako mvutano uliotokea tena na migongano iliyoripotiwa vimesababisha mazingira mabaya zaidi ya usalama.
Katibu Mkuu huyo ametoa wito wa kutekelezwa kikamilifu Makubaliano ya Kudumu ya Kusitisha Mapigano, na kusisitiza umuhimu wa kulinda yaliyofikiwa tangu mwaka 2022.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



