Vikaangio na Ndoto: Vijana wa Tanzania Wakumbatia Sanaa ya Upishi wa Kichina

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 02, 2026

Wanafunzi wa Tanzania wakijifunza kupika baozi kwa mvuke huko Dar es Salaam, Tanzania, Januari 28, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Wanafunzi wa Tanzania wakijifunza kupika baozi kwa mvuke huko Dar es Salaam, Tanzania, Januari 28, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

DAR ES SALAAM – Ndani ya jiko lenye pilikapilika nyingi katikati ya jiji la Dar es Salaam, Ruth Washima Seni, mwanafunzi kijana wa mambo ya hoteli nchini Tanzania, anajaribu kukata viazi mviringo katika vipande vyembamba kama nywele.

Hii ni mbinu ya mkato wa "sindano ya silva" (silver needle), jaribio gumu la ustadi wa kutumia kisu katika upishi wa Kichina. Seni ni mmoja wa wanafunzi 20 katika kundi la hivi karibuni la programu ya kipekee ya mapishi katika Chuo cha Teknolojia na Usimamizi cha Kilimanjaro (KITM). Programu hiyo, iliyozinduliwa Januari 2026, ni ushirikiano kati ya chuo hicho na "The Best Company," kampuni ya China inayojikita katika shughuli za kubadilishana utamaduni.

Ikiongozwa na Mpishi Mahiri Wang Bo kutoka Mkoa wa Sichuan wa China, mtaala huo unahusisha ladha ya pilipili ya vyakula vya Sichuan, ladha nzuri ya mchuzi wa kaskazini-mashariki mwa China, na ladha freshi ya vyakula vya Kikantoni.

Msukumo mkuu kwa vijana hawa wanaokimibiza ndoto ni fursa za kiuchumi.

Filbert Haule, mkufunzi wa mambo ya hoteli katika KITM, ameeleza kuwa uamuzi wa kuanzisha mafunzo hayo ya upishi wa Kichina ulikuwa wa kimkakati. Wakati ambapo watalii na wafanyabiashara wa China wanazidi kutoa mchango unaoonekana katika uchumi wa Tanzania, mahitaji ya chakula halisi cha Kichina yanaongezeka.

Aidha, Tanzania inajiandaa kupokea idadi kubwa ya watalii wa kimataifa wakati huu ambao inajiandaa kuwa moja ya wenyeji wa mashindano ya soka ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027.

"Tunataka kuwapa watalii ladha mpya" Haule amesema. "Wakati wawekezaji na wamiliki wa migahawa wanapoona kwamba wanafunzi hawa wanaweza kupika chakula halisi na kitamu cha Kichina, watavutiwa. Hii inatengeneza fursa zaidi."

Kwa Mpishi Wang, chakula ni balozi wa msingi. "Chakula ni daraja linalounganisha watu," amesema. "Wanafunzi wanapoelewa utamaduni, wanapika kwa hisia, na vyakula hufikia kiwango cha juu zaidi.”

Wahitimu wa programu hii wanapendekezwa kwa migahawa na hoteli za Kichina kote katika eneo hilo, jambo linalowapa njia ya haraka ya kupata ajira.

Wanafunzi wa Tanzania wakijifunza mbinu ya mkato wa “sindano ya silva”, jaribio gumu la ustadi wa kukata kwa kisu katika upishi wa Kichina, mjini Dar es Salaam, Tanzania, Januari 28, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Wanafunzi wa Tanzania wakijifunza mbinu ya mkato wa "sindano ya silva", jaribio gumu la ustadi wa kukata kwa kisu katika upishi wa Kichina, mjini Dar es Salaam, Tanzania, Januari 28, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha