Lugha Nyingine
Msumbiji yazindua kiwanda cha kuchakata grafiti kilichojengwa na China; Rais Chapo apongeza uongezaji thamani

Picha hii iliyopigwa Januari 31, 2026 ikionyesha kiwanda cha kuchakata grafiti kilichojengwa na Kampuni ya China katika Wilaya ya Nipepe, mkoa wa Niassa, Msumbiji. (Xinhua/Liu Jie)
MAPUTO - Kiwanda cha kuchakata grafiti kilichowekezwa na kujengwa na Kampuni yenye mtaji wa China ya Jinan Yuxiao kimezinduliwa rasmi Ijumaa katika Wilaya ya Nipepe, mkoa wa Niassa, kaskazini mwa Msumbiji.
Katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho siku ya Ijumaa, Rais wa Msumbiji Daniel Francisco Chapo alitoa salamu kwa wawakilishi wa DH Grafite na jumuiya ya wafanyabiashara wa China waliokuwapo, akiwapongeza kwa imani waliyoonyesha kwa Msumbiji pamoja na dhamira yao ya vitendo katika uzalishaji na uchakataji nchini humo.
Mradi huo ulianzishwa na kuwekezwa na kampuni ya China ya Jinan Yuxiao, ukiwa na uwekezaji wa jumla wa takriban dola milioni 150 za Marekani. Unahusisha uchimbaji madini, uongezaji thamani na uchakataji, na umesanifiwa kuwa na uwezo wa kuchakata tani 200,000 za grafiti kwa mwaka.
Rais Chapo, Waziri wa Rasilimali Madini na Nishati wa Msumbiji Estevao Rafael Pale, na wawakilishi wa serikali ya mkoa wa Niassa walihudhuria hafla hiyo.
Rais Chapo amesema kwamba zaidi ya kuzindua kiwanda hicho cha uzalishaji, hafla hiyo inaakisi maono ya nchi inayojiondoa kutoka kuwa muuzaji tu wa malighafi, na badala yake kujipanga kuwa mzalishaji, msindikaji na muuzaji nje wa bidhaa zenye thamani iliyoongezwa, hatua inayotoa ajira kwa watu wake, kuongeza mapato ya familia na kuleta maendeleo nchini Msumbiji.
Wakati wa utekelezaji wa mradi, kampuni hiyo iliwekeza katika ujenzi wa daraja la kuvuka Mto Lurio katika mkoa wa Niassa na kujenga takriban kilomita 100 za barabara, kuunganisha eneo la Nipepe na mtandao wa kitaifa wa usafiri. Aidha, takriban kilomita 100 za njia za kusambaza umeme wa kilovolti 110 zilijengwa ili kuhakikisha upatikanaji wa umeme thabiti na wa kuaminika kwa wakazi wa eneo hilo na maendeleo ya kikanda.
Wu Tao, mwenyekiti wa Kampuni ya Jinan Yuxiao, amesema mradi huo umeajiri zaidi ya wafanyakazi wenyeji 800, na kwamba kwa kuendelea kwa awamu ya pili ya mradi huo, jumla ya ajira zinatarajiwa kuzidi 2,000. Ameongeza kuwa programu za mafunzo ya kimfumo zitatekelezwa ili kuinua ujuzi wa wafanyakazi na kusaidia kuongeza mapato na kuboresha hali ya maisha ya wenyeji.

Picha hii iliyopigwa Januari 30, 2026 ikionyesha nyumba mpya zilizojengwa na Kampuni ya Jinan Yuxiao ya China katika Wilaya ya Nipepe, mkoa wa Niassa, Msumbiji. (Xinhua/Liu Jie)

Picha hii iliyopigwa Januari 31, 2026 ikionyesha kiwanda cha kuchakata grafiti kilichojengwa na Kampuni ya Jinan Yuxiao ya China katika Wilaya ya Nipepe, mkoa wa Niassa, Msumbiji. (Xinhua/Liu Jie)

Picha hii iliyopigwa Januari 30, 2026 ikionyesha mstari wa uzalishaji wa kiwanda cha kuchakata grafiti kilichojengwa na Kampuni ya Jinan Yuxiao ya China katika Wilaya ya Nipepe, mkoa wa Niassa, Msumbiji. (Xinhua/Liu Jie)

Rais wa Msumbiji Daniel Francisco Chapo akitembelea kiwanda cha kuchakata grafiti kilichojengwa na Kampuni ya Jinan Yuxiao ya China katika Wilaya ya Nipepe, Mkoa wa Niassa, Msumbiji, Januari 30, 2026. (Xinhua/Liu Jie)

Watu wakitembea kwenye daraja la kuvuka Mto Lurio, lililojengwa na Kampuni ya Jinan Yuxiao ya China, katika Wilaya ya Nipepe, Mkoa wa Niassa, Msumbiji, Januari 31, 2026. (Xinhua/Liu Jie)

Picha hii iliyopigwa Januari 31, 2026 ikionyesha kiwanda cha kuchakata grafiti kilichojengwa na kampuni ya China katika Wilaya ya Nipepe, Jimbo la Niassa, Msumbiji. (Xinhua/Liu Jie)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



