Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa wito wa ushirikiano na Uruguay katika sekta mbalimbali

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Uruguay Yamandu Orsi, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Februari 3, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - China na Uruguay zinapaswa kuimarisha mafungamano ya mikakati ya maendeleo, na kuzidisha ushirikiano katika sekta za uchumi na biashara, mambo ya fedha, kilimo na ufugaji wa mifugo, ujenzi wa miundombinu, na teknolojia ya kupashana habari na mawasiliano, Rais wa China Xi Jinping alisema Jumanne wakati akifanya mazungumzo na Rais wa Uruguay Yamandu Orsi mjini Beijing.
Rais Orsi Jumapili alianza ziara ya kiserikali ya wiki moja nchini China. Ni kiongozi wa kwanza kutoka Latini Amerika kufanya ziara China katika mwaka 2026, na kabla ya ziara yake hiyo, viongozi kutoka Ireland, Korea Kusini, Canada, Finland na Uingereza walifanya ziara nchini China.
Rais Xi amesema: "Katika siku hii ya miaka 38 iliyopita, China na Uruguay zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia." Alibainisha kuwa katika miaka mingi iliyopita, bila kujali mabadiliko katika hali ya kimataifa, nchi hizo mbili siku zote zinadumisha uhusiano wa kirafiki kwenye msingi wa kuheshimiana na kufanya ushirikiano wa kunufaishana.
Rais Xi ametoa wito kwa pande zote mbili kuendeleza desturi zao na kuzidisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote katika hali mpya, ili kuhakikisha urafiki wao unakuwa imara zaidi na wenye nguvu hai zaidi.
"China na Uruguay zinapaswa kuendelea kuungana mkono kithabiti katika maslahi ya msingi na masuala makuu yanayofuatiliwa ya kila mmoja, kuimarisha mawasiliano ya kirafiki kwenye ngazi zote na katika sekta mbalimbali, kuongeza kubadilishana mawazo kuhusu uzoefu katika utawala wa nchi, na kuzidisha hali ya kuaminiana kimkakati," Rais Xi amesisitiza.
Rais Orsi amesema kuwa Uruguay inaunga mkono kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na kuunga mkono sera ya "nchi moja, mifumo miwili", na Uruguay inatamani kuzidisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote na China na kuendeleza ushirikiano wa pande mbili kwenye kiwango cha juu zaidi.
Akiitikia wito wa Rais Xi, Rais Orsi ametoa wito wa kuimarisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali mapana ili kuingiza msukumo imara zaidi kwenye uhusiano kati ya Uruguay na China na kuleta manufaa makubwa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Uruguay Yamandu Orsi kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kabla ya mazungumzo yao Februari 3, 2026. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Uruguay Yamandu Orsi, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Februari 3, 2026. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Uruguay Yamandu Orsi kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kabla ya mazungumzo yao, Februari 3, 2026. (Xinhua/Yan Yan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



