Rais Xi atoa wito kwa China na Russia kukuza uhusiano na kushirikiana kudumisha utulivu wa kimkakati duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 05, 2026

Rais wa China Xi Jinping akifanya mkutano wa mtandaoni na Rais wa Russia Vladimir Putin katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 4, 2026. (Xinhua/Liu Bin)

Rais wa China Xi Jinping akifanya mkutano wa mtandaoni na Rais wa Russia Vladimir Putin katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 4, 2026. (Xinhua/Liu Bin)

BEIJING - China na Russia zinapaswa kuongeza mawasiliano ya ngazi ya juu na kuimarisha ushirikiano wa kivitendo katika nyanja mbalimbali, Rais Xi Jinping wa China amesema kwenye mkutano wa mtandaoni na mwenzake wa Russia Vladimir Putin jana Jumatano.

Rais Xi ametoa salamu za Mwaka Mpya kwa Rais Putin na watu wa Russia, akisema kwamba siku hiyo ya Jumatano ilikuwa ni Mwanzo wa Majira ya Mchipuko kwenye kalenda ya kilimo ya China, ambayo inawakilisha mwanzo mpya. Katika siku hiyo nzuri, Rais Xi ameeleza utayari wake wa kushirikiana na Rais Putin ili kuweka dira mpya kwa uhusiano wa pande mbili.

Rais Putin amemtakia Rais Xi na watu wa China sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China yenye furaha, nguvu hai kubwa na mafanikio katika juhudi zote.

Akibainisha kuwa mikutano yao miwili mwaka jana iliimarisha uhusiano kati ya China na Russia katika awamu mpya ya maendeleo, Rais Xi amesema nchi hizo mbili ziliadhimisha miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, zilidumisha mawasiliano makubwa ya kiuchumi na biashara, kudumisha mawasiliano na ushirikiano wa watu na watu, na kuendelea kujitolea kujenga mfumo wa usimamizi duniani ulio wa haki na usawa zaidi.

Huku akieleza kwamba mwaka huu ni mwanzo wa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa China, Rais Xi amesisitiza kwamba nchi hiyo itakuwa ikichukua hatua makini za mapema katika kupanua ufunguaji mlango wake wa ngazi ya juu na itashiriki fursa mpya za maendeleo na nchi kote duniani, ikiwemo Russia.

Rais Xi amesema nchi hizo mbili zinapaswa kuhakikisha kwamba uhusiano wa pande mbili unazidi kuendelea kwenye njia sahihi kupitia kuimarisha uratibu wa kimkakati na kutekeleza kikamilifu majukumu ya nchi kubwa kwa mtazamo wa kuwajibika.

"Zikiwa ni nchi kubwa zenye kuwajibika na wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, China na Russia zina wajibu wa kuhimiza jumuiya ya kimataifa kushikilia haki na usawa, kulinda kithabiti matokeo ya ushindi wa Vita vya Pili vya Dunia, na kutetea kwa uthabiti mfumo wa kimataifa unaozingatia Umoja wa Mataifa na kanuni za msingi za sheria za kimataifa," ameongeza.

Huku akieleza imani yake kamili katika uhusiano kati ya Russia na China, Rais Putin amesema kwamba pande zote mbili zinapaswa kuendelea kuungana mkono kithabiti katika kulinda mamlaka na usalama wao wa taifa, na katika kufikia maendeleo na ustawi wa kiuchumi na kijamii.

"Pia zinapaswa kukuza elimu na mawasiliano ya kiutamaduni ili kunufaisha watu wa nchi hizo mbili," ameongeza.

"Ikikabiliwa na hali ngumu na inayobadilika ya kimataifa, Russia ina nia ya kuendelea kuimarisha uratibu wa kimkakati na China kwenye majukwaa ya pande nyingi kama vile Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na BRICS, na hivyo kuingiza nishati chanya katika masuala ya kimataifa" Rais Putin amesema.

Rais wa China Xi Jinping akifanya mkutano wa mtandaoni na Rais wa Russia Vladimir Putin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 4, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha