Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar atarajia uhusiano kati ya nchi hiyo na China kuonesha uhai mpya katika mwaka mpya

(CRI Online) Februari 09, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar, Christine Razanamahasoa, anatoa hotuba kwenye hafla za vyakula vitamu vya China kwa kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China mjini Antananarivo, Madagascar, Februari 7, 2026. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Waziri wa Mambo ya nje wa Madagascar Christine Razanamahasoa amesema anatarajia uhusiano kati ya nchi hiyo na China utaonesha uhai mpya katika mwaka mpya, na pia ametoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa watu wa China.

Razanamahasoa amesema hayo alipohudhuria hafla ya uzinduzi wa shughuli za Mwaka wa Mawasiliano ya Kitamaduni kati ya China na Afrika zilizofanyika huko Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar.

Katika hafla hiyo, Razanamahasoa pia amesema Madagascar iko tayari kushirikiana na China kuimarisha uaminifu kwa pande zote, kupanua ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, kukuza mawasiliano ya kitamaduni, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha