Lugha Nyingine
Watanzania na Wachina wanaoishi Tanzania washerehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China mjini Dar es Salaam

Mgeni Mtanzania na mtoto wa China wakijaribu kuandika maandiko ya Kichina kwenye Ubalozi wa China huko Dar es Salaam, Tanzania, Februari 6, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)
DAR ES SALAAM, Februari 7 -- Watanzania na Wachina wanaoishi Tanzania walikusanyika katika Ubalozi wa China nchini Tanzania Ijumaa iliyopita wakisherehekea pamoja Sikukuu inayokaribia ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.
Katika shughuli hiyo, wajumbe wa wanadiplomasia, maofisa wa serikali na wajumbe wa jamii walikusanyika pamoja wakionyesha urafiki unaokuwa mkubwa zaidi kati ya nchi hizo mbili. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, James Kinyasi Millya, akiwa kwa niaba ya serikali ya Tanzania alitoa salamu za kikunjufu kwa wananchi wa China na Wachina wanaoishi ng'ambo.
Millya aliushukuru Ubalozi wa China kwa kuandaa shughuli hiyo, alisema kuwa shughuli kama hiyo ya kufanya maingiliano ya kiutamaduni yameongeza mawasliano kati ya watu wa nchi hizo mbili.
Millya alisema kuwa, katika mwaka uliopita, Tanzania na China zimepata maendeleo makubwa kwa kupitia mawasiliano na ushirikiano ulioongezeka zaidi kati ya viongozi, taasisi na watu wa nchi hizo mbili.
Millya alisema kuwa China ni moja ya wenzi wa kimkakati muhimu zaidi kwa Tanzania. Pia amekaribisha mawasiliano wa kiuchumi yanayozidi kuwa karibu siku hadi siku, akitaja upanuzi wa biashara, uwekezaji unaoongezeka kutoka China, pamoja na maendeleo ya mawasiliano yanayoendelea katika hali motomoto kwenye sekta za utamaduni na elimu.
Pia alisema kuwa mwaka 2026 umetangazwa kuwa ni Mwaka wa Mawasiliano kati ya Watu na Watu wa China na Afrika, ambapo fursa mpya zitaletwa kwa kuimarisha ushirikiano katika sekta za utamaduni, elimu, maendeleo ya teknolojia na shughuli za utalii.
Kaimu Balozi wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Wang Yong akihutubia shughuli hiyo, alisema kuwa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China inaonesha kujumuika kwa wanafamilia, nguvu hai na matumaini.
Wang alisema kuwa uhusiano kati ya China na Tanzania unaendelea kukua kwa kina, hali ya kuaminiana kisiasa imekuwa ya karibu zaidi, ushirikiano wa kiuchumi unapanuka hatua kwa hatua, na mawasiliano ya kiutamaduni yanaongezwa kwa kina siku hadi siku.

Watanzania na Wachina wanaoishi Tanzania wakifurahia pamoja vyakula vitamu huko Dar es Salaam, Tanzania, Februari 6, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



