Lugha Nyingine
Vijana wa nchi za Kusini ya Dunia watafiti njia za maendeleo za Mkoa wa Yunnan, China

Watu kutoka nchi za Kusini ya Dunia wakipiga picha pamoja katika Kijiji cha Hebian cha Wilaya ya Mengla ya Mkoa wa Yunnan, China Desemba 5, 2025. (Picha/Xinhua)
KUNMING – Hivi karibuni, kundi la vijana kutoka nchi za Indonesia, Kenya, Laos, Tanzania na Uganda walitembea kwa miguu kuingia kwenye sehemu ya milimani inayofunikwa na miti na mimea mkoani Yunnan, kusini-magharibi mwa China. Vijana hao si watalii wa kawaida, walikuwa wanafunzi katika mafunzo ya "Darasa la Maisha" yanayofuatilia maendeleo ya vijijini.
"Shule" yao ilikuwa katika Kijiji cha Hebian cha Wilaya ya Mengla kilicho karibu na mpaka kati ya China na Laos, ambako watu wengi wa kabila wa Wayao wanaishi huko. Kijiji cha Hebian kilikuwa na hali ya umaskini zaidi, lakini hivi sasa kimebadilika kuwa "kijiji nyota," kikiwapokea maelfu ya maofisa, wasomi, wataalamu, na vijana kutoka nchi mbalimbali za Kusini ya Dunia.
Katika kijiji hicho, nyumba za kijadi za mbao za Wayao zimejengwa upya na kubadilika kuwa vyumba vya kuwapokea wageni, kumbi za mikutano, na baa za kijijini. Mtindo huu umeziwezesha shughuli za utalii za kisasa kufungamana kikamilifu na maisha ya watu wa kijiji hicho.
Byaruhanga Emmanuel Abwooli, mshiriki kutoka Uganda, alipoona vyumba vya sifa bora vya wageni vinavyoendeshwa na wanakijiji vilichangia mapato yao kuongezeka kwa mara dufu, alisema, aliyoona si tu ni faida, bali ni mpango wa utatuzi wa masuala. Abwooli alisema kuwa nchini Uganda, mashamba mengi ya familia yanakabiliwa na hatari kubwa za magonjwa na usimamizi mbovu. Alisema, mtindo wa China wa kuunganisha ufugaji wa kijadi na sayansi ya kisasa ya usalama wa viumbe pamoja na kilimo cha mzunguko, na kutoa njia inayowekwa wazi na inayoweza kutekelezeka kwa ajili ya kutimiza lengo la kuhifadhi mazingira ya asili na kujipatia ufanisi mkubwa zaidi.
Kwa washiriki wengi, teknolojia ya hali ya juu katika kilimo cha kisasa cha China kiliwashangaza sana. Al Fiqie, mjasiriamali kijana kutoka Indonesia, alitembelea kituo cha huduma za kilimo ambako droni kubwa na matrekta ya teknolojia ya kisasa yako tayari kufanya kazi kwenye mashamba ya kitropiki.
Fiqie alisema kuwa teknolojia inafanya kilimo kiwe na nguvu bora sana, akiongeza kuwa mustakabali wa nchi za Kusini ya Dunia upo katika mafungamano ya teknolojia na mambo ya kijadi.
Maendeleo ya Yunnan ni mfano mzuri wa mchakato wa ustawishaji wa vijiji nchini China. Yunnan ukiwa mkoa wenye makabila madogo mengi zaidi na hali ya utatanishi zaidi ya ardhi nchini China , umefanikiwa kuwasaidia wanavijiji milioni 9.33 kuondokana na umaskini. Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka jana, wastani wa mapato ya kila mtu yanayoweza kutumika mkoani Yunnan ulifikia Yuan 31,311 (karibu dola za Marekani 4,513).

Watu kutoka nchi za Kusini ya Dunia wanatembelea kijiji cha Hebian cha Wilaya ya Mengla ya Mkoa wa Yunnan, China Desemba 5, 2025. (Picha/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



