Lugha Nyingine
Uganda yakaribisha mwaka wa mawasiliano kati ya watu wa China na Afrika kwa maonyesho ya biashara na sanaa
Picha hii ni onyesho la fataki kwenye hafla ya uzinduzi wa Mwaka wa Mawasiliano kati ya watu wa China na Uganda na kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, jijini Kampala, Uganda, Februari 8, 2026. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)
Uganda imezindua mwaka wa mawasiliano kati ya watu wa China na Uganda kwa maonyesho ya kukaribisha mwaka mpya wa jadi wa China.
Makamu wa Rais wa Uganda, Bibi Jessica Alupo, alikuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo, na alizindua rasmi mwaka huo baada ya kutembelea mabanda yaliyoonyesha bidhaa na huduma za China na Uganda, ikiwa ni pamoja na mashine nzito, vyakula vya jadi na huduma za utalii.
Bibi Alupo amesema ushirikiano kati ya China na Uganda umeleta manufaa kwa pande zote mbili, na kuishukuru China kwa msaada inaotoa kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu, ufadhili wa elimu na programu za ujenzi wa uwezo.
Pia amesema mawasiliano kati ya watu wa pande mbili yanajenga msingi thabiti wa ushirikiano wa kudumu, ndio maana mwaka 2026 umetengwa kuwa mwaka wa mawasiliano ya watu kati ya China na Afrika.
Makamu wa Rais wa Uganda Jessica Alupo akisaini kwenye mchoro wa farasi kwenye hafla ya uzinduzi wa Mwaka wa Mawasiliano kati ya watu wa China na Uganda na kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, jijini Kampala, Uganda, Februari 8, 2026. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)
Wasanii wa Uganda wanaocheza kwenye hafla ya uzinduzi wa Mwaka wa Mawasiliano kati ya watu wa China na Uganda na kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, jijini Kampala, Uganda, Februari 8, 2026. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



