Lugha Nyingine
Rais wa Kenya aahidi kuimarisha uhusiano na jamii ya kimataifa kuendeleza amani
Rais wa Kenya William Ruto ameahidi kupanua na kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na jamii ya kimataifa katika mwaka huu wa 2026.
Rais Ruto amesema hayo katika hotuba yake ya mwaka kwa Wakuu wa Mabalozi na Mashirika ya Kimataifa aliyoitoa jana katika mji wa Nairobi. Amesema Kenya itaendeleza mifumo ya ushirikiano wa pande mbili wa kimataifa, kuboresha amani na usalama, kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji, kupanua mabadilishano ya kisayansi, kiteknolojia na kiutamaduni, kuendeleza maingiliano ya kikanda, kuwezesha uhamaji wa nguvu kazi, na kuboresha juhudi za pamoja kuelekea maslahi ya pamoja ya bara la Afrika na maslahi ya pande nyingi.
Rais Ruto amesema, licha ya mchango mkubwa katika ajenda na jukumu la ulinzi wa amani la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuendelea kutengwa kwa bara la Afrika kunadhoofisha uhalali na ufanisi wa Umoja wa Mataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



