Lugha Nyingine
Ripoti ya Usalama wa Munich 2026 yatoa onyo kuhusu “siasa za kiuharibifu” zinazovuruga utaratibu wa kimataifa
Mwenyekiti wa Mkutano wa Usalama wa Munich Wolfgang Ischinger akishiriki kweye shughuli ya utoaji wa Ripoti ya Usalama ya Munich 2026 huko Berlin, German, Februari 9, 2026. (Xinhua/Li Chao)
BERLIN, Februari 9 — “Ripoti ya Usalama wa Munich 2026” iliyotolewa jana Jumatatu ikisema, Dunia imeingia katika kipindi cha “siasa za kiuharibifu,” ambapo uharibifu mkubwa umekuwa hali ya kawaida. .
Ripoti hiyo yenye kichwa cha “Chini ya Uharibifu” inalenga kuweka utoaji maoni ya kimsingi wa Mkutano wa Usalama wa Munich (MSC) utakaofanyika wiki hii. Siku chache baadaye wiki hii, wakuu karibu 50 wa nchi na serikali pamoja na mamia ya watoa maamuzi na viongozi wa maoni wanatazamiwa kuhudhuria kwenye mkutano huo wa kila mwaka.
Ripoti hiyo imesema, serikali ya Marekani ya hivi sasa inachukuliwa kuwa ni mtendaji anayejitokeza zaidi, ambayo imeahidi kujitoa kutoka vizuizi vya utaratibu uliopo sasa, na hii imefanya utaratibu wa baada ya Vita vya Pili vya Dunia unaoongozwa na Marekani kukabiliwa na hali ya kusambaratika.
Ripoti hiyo pia imesema kuwa katika jamii nyingi za nchi za Magharibi, nguvu za kisiasa zinazoelekea uharibifu badala ya mageuzi zinaimarika zaidi, na chanzo chake ni kukata tamaa kwa utendaji wa taasisi za kidemokrasia na kutoamini marekebisho ya misimamo ya kisiasa.
Ripoti hiyo imeonya kwamba dunia huenda itaona ushirikiano unaofanywa kwenye msingi wa kanuni utabadilika kuwa biashara ya kimaslahi, na kutafuta maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma, na hali ya umwamba wa kikanda itaonekana badala ya hali ya kufuata utaratiba katika maeneo mengi duniani.
Waandalizi wa Mkutano wa Usalama wa Munich wakionyesha Ripoti ya Usalama ya Munich 2026 huko Berlin, German, Februari 9, 2026. (Xinhua/Li Chao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



