Nyaraka mpya za Epstein zaongeza msukosuko wa kisiasa katika nchi nyingi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 10, 2026

Picha iliyopigwa tarehe 17, Novemba, 2025 ikionyesha Bunge la Marekani huko Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Hu Yousong)

Picha iliyopigwa tarehe 17, Novemba, 2025 ikionyesha Bunge la Marekani huko Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Hu Yousong)

BEIJING, Februari 9 – Nyaraka mpya zilizotolewa hadharani kuhusu Jeffrey Epstein, mtaalamu wa mambo ya fedha aliyefariki dunia, zimesababisha uchunguzi katika Ulaya na Marekani, na kusababisha wanasiasa kadha wa kadha kujiuzulu kwa kuhusika na mhalifu huyo wa ngono aliyehukumiwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Jumapili iliyopita ya Sky News, katika nchi ya Uingereza, Morgan McSweeney amejiuzulu wadhifa wa mkuu wa ofisi ya Waziri Mkuu Keir Starmer, baada ya kushtakiwa na kutakiwa kuwajibika kwa kumteua Peter Mandelson kuwa balozi wa Uingereza nchini Marekani,

Mandelson mwenye umri wa miaka 72, aliteuliwa kuwa balozi wa Uingereza huko Washington mwanzoni mwa mwaka 2025. Starmer alimfukuza kazini baada ya miezi saba tu kwa sababu ya athari zilizotokana na kuhusika na Epstein katika nyaraka zilizofichuliwa.

Alhamisi iliyopita, Starmer pia aliomba radhi kwa uamuzi wake wa kumteua Mandelson kuwa balozi, akisema kwamba amepuuza hali mbaya ya uhusiano uliokuwepo kati ya Mandelson na Epstein.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vimetoa habari vikisema kuwa , siku ya Jumamosi iliyopita, Waziri wa zamani wa Utamaduni wa Ufaransa Jack Lang, aliomba kujiuzulu wadhifa wake wa mwenyekiti wa Taasisi ya Dunia ya Kiarabu, ambayo ni taasisi ya utamaduni na elimu yenye makao makuu huko Paris, kutokana na mkwaruzano kuhusu kuhusika na nyaraka mpya za kesi ya Epstein.

Tarehe 30, Januari, Wizara ya Sheria ya Marekani ilisema kuwa imetoa mamilioni ya kurasa mpya za nyaraka kwa kufuata “Sheria ya Uwazi wa Nyaraka za Epstein” (“Epstein Files Transparency Act”), na nyaraka hizo zimefikia karibu kurasa milioni 3.5, pamoja na maelfu ya video na picha. Kutolewa hadharani kwa nyaraka nyingi zaidi kumeongeza uchunguzi zaidi juu ya mfumo wa uhusiano na Epstein na kuongeza shinikizo jipya la kisiasa katika nchi nyingi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Lavrov, alisema Jumapili iliyopita kwamba nyaraka hizo zimefichua “ushetani kamili” wa watu wa tabaka la juu wa nchi za Magharibi na kuonesha sura halisi ya shirikisho la kisiri la Magharibi ya kujaribu kutawala dunia nzima.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha