Ripoti: Iran yaweza kupunguza uranium iliyorutubishwa ikiwa vikwazo vyote vitaondolewa

(CRI Online) Februari 10, 2026

Shirika la habari la kitaifa la Iran IRNA jana Jumatatu limeripoti kwamba, mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran Bw. Mohammad Eslami amesema, nchi hiyo inaweza kupunguza uranium yake iliyorutubishwa ikiwa vikwazo vyote dhidi yake vitaondolewa.

Alipojibu swali kwamba kama Marekani imetaka Iran kupunguza uranium yake iliyorutubishwa kwa 60%, Bw. Eslami alisema kwamba, hatua hiyo inategemea kama Marekani itaondoa vikwazo vyote kama sharti.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha