Sudan yasema itarejea IGAD baada ya kusitisha uanachama wake kwa zaidi ya miaka miwili

(CRI Online) Februari 10, 2026

Sudan imetangaza kuwa itarejea tena kikamilifu katika shughuli zinazohusiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD), na kumaliza mvutano wa kidiplomasia ulioanza zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan kwa vyombo vya habari imesema, uamuzi wa kurejea katika shirika hilo la kikanda la Afrika Mashariki umefuatia mabadiliko chanya ya Sekretarieti ya IGAD.

Hatua hiyo inaashiria mabadiliko makubwa kwa Sudan, ambayo Januari, 2024, ilisitisha uanachama wa IGAD, na kuituhumu kuweka ajenda ya mgogoro wa Sudan katika mkutano wake bila ya majadiliano ya awali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha