Wataalamu wakutana Kenya kujadili uwekezaji wa sekta binafsi kuboresha sekta ya chakula barani Afrika

(CRI Online) Februari 10, 2026

Wataalamu wamekutana jana katika Nairobi, mji mkuu wa Kenya, kujadili njia za kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi ili kuongeza kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo barani Afrika.

Mjadala wa siku mbili wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kuhusu kuhamasisha sekta binafsi kwa biashara na uwekezaji endelevu katika sekta ya chakula ya Afrika, ulikutanisha zaidi ya wajumbe 100, wakiwemo maofisa wa serikali, wakuu wa viwanda, na wawakilishi kutoka mashirika ya kiuchumi ya kikanda.

Mkurugenzi wa kitengo cha sekta binafsi katika Sekretariet ya Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) Themba Khumalo amesema, bara hilo litahamasisha uwekezaji binafsi kwa kuwa unatoa jukwaa la kufungua fursa kubwa ya kilimo barani Afrika kupitia biashara.

Aliyekuwa makamu wa rais wa Nigeria Yemi Osinbajo amesema, wawekezaji binafsi wanaweza kuunga mkono serikali za Afrika katika kuwezesha wakulima wadogo kukabiliana na changamoto za pande mbalimbali, kama vile upatikanaji wa huduma za mikopo nafuu na uenezaji wa bidhaa za kilimo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha